30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simbu apania medali mbio za Tokyo

Mwanariadha Alphonce Simbu, akilakiwa na mkewe Rehema, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana, akitokea nchini Brazil kwenye michuano ya Kimataifa ya Olimpiki.
Mwanariadha Alphonce Simbu, akilakiwa na mkewe Rehema, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Dar es Salaam jana, akitokea nchini Brazil kwenye michuano ya Kimataifa ya Olimpiki.

Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM

MWANARIADHA wa Tanzania aliyeibuka shujaa kwa kushika nafasi ya tano katika mbio ndefu (marathon) kwenye michezo ya Olimpiki mwaka huu, Alphonce Simbu, ameitaka Serikali kuanza mara moja harakati za kusaka medali mwaka 2020 michezo hiyo itakapofanyika jijini Tokyo, Japan.

Simbu alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akitokea jijini Rio de Jeneiro, nchini Brazil alikokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki.

Alisema asilimia kubwa ya wanamichezo waliofanya vizuri katika michezo ya Olimpiki mwaka huu waliandaliwa vyema na nchi zao tofauti na ilivyokuwa kwa upande wake.

“Wenzetu waliandaliwa vyema, mimi naamini uwezo wa Tanzania kupata medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki upo, lakini endapo Serikali itaanza kampeni ya kutimiza lengo hilo kuanzia sasa na si kusubiri michezo inapokaribia,” alisema Simbu.

Aidha, Simbu aliongeza kwamba haikuwa kazi rahisi kwake kushika nafasi ya tano kama watu wanavyodhani kwa kile alichodai kuwa akiwa katika mbio ndefu ‘marathon’ alichuana vikali na wanariadha mashuhuri na wakongwe waliokuwa na uchu wa kupata medali.

“Changamoto ambayo sitaweza kuisahau ni pale nilipofika umbali wa km 20 nikiwa karibu kabisa na Mkenya, Kipchoge Eliud (mshindi wa mbio hizo) kwa kweli hapo ndipo niliona mbio ni ngumu.

“Kipchoge alikuwa anakimbia mwendo kasi ajabu na endapo ningefuata nyayo zake hakika nisingefika popote na badala yake ningeishia kuwa mtu wa mwisho kabisa. Lakini niliamua kwenda na kasi niliyoanza nayo na hatimaye kuwapita wenzangu zaidi ya 100,” alisema.

Mwanariadha huyo kijana aliyeshiriki michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza, alikimbia mbio za marathon akitumia muda wa saa 2:11:15, ambapo aliwashukuru Watanzania, Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kwa sapoti waliyompa kufanikisha ushindi wake.

Naye Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alisema kamati hiyo kwa kushirikiana na RT itaandaa mpango mkakati kuhakikisha wanariadha wengi zaidi wanashiriki mbio za kimataifa zikiwamo ya Nyika na zile za dunia zitakazofanyika mwakani kama sehemu ya maandalizi ya Olimpiki ya mwaka 2020.

Kwa upande wake mwanariadha mkongwe, Juma Ikangaa ambaye aliwahi kushika nafasi ya sita mwaka 1984 na nafasi ya saba mwaka 1988 katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Soul, Korea, aliwataka Watanzania kuacha kubeza ushindi wa Simbu.

Shujaa huyo aliwasili nchini saa 9 alasiri akiambatana na wanariadha wenzake ambao ni Saidi Makula aliyeshika nafasi ya 43 na Fabiano Joseph aliyemaliza nafasi ya 112.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles