30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Simba watoa vifaa vya corona Muhimbili

 MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM 

KLABU ya Simba kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji, wamekabidhi msaada wa vizimba vya kuosha mikono, sabuni pamoja na vitakasa mikono (sanitizer) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kusaidia kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona. 

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha, wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa sekta nzima ya afya na hivyo wameona wachangie sabuni pamoja na vitakasa mikono ili kuweza kukabiliana na virusi vya corona.

Kwa upande wao, Mkurugenzi wa MNH Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi wa MOI, Dk. Samuel Swai na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya ya Moyo wa JKCI, Dk. Tulizo Shemu, wameshukuru kwa msaada huo kwa kuwa utasaidia kupunguza kazi ya usimamizi wa kuosha mikono ambayo mwanzo ilibidi ifanyike na walinzi katika milango mikuu na milango ya kuingia majengo yote ya hospitali.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez, alisema kuwa ujenzi wa vizimba hivyo ambavyo ni zaidi ya 50 ni mwanzo wa zoezi ambalo litaendelea katika hospitali nyingine kama Mloganzila, Mwananyamala, Temeke na Amana.

Alisema wanatumia nafasi hiyo kwa kuwashukuru uongozi wa hospitali zote tatu na kila mmoja katika kufanya kazi, kufanikisha zoezi hilo licha ya kuwa na changamoto ya ugonjwa wa Covid-19.

Aliongeza kuwa wataendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwamo barakoa na vitakasa mikono katika hospitali nyingine za jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles