30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Simba, Messi wafikia pabaya

MESSI GOALNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM
UTATA wa mkataba wa winga Ramadhan Singano ‘Messi’ na timu yake ya Simba sasa umefikia pabaya, baada ya pande hizo mbili kufikiria kushtakiana ili kusaka suluhu.
Wakati Messi akisaka ufumbuzi wa suala hilo kwenye Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza), uongozi wa Simba unataka kumshtaki kama akiendelea kuichafua klabu hiyo kwenye vyombo vya habari.
Winga huyo bado hajakubaliana na Simba kuhusu kusaini mkataba mpya baada ya kudai mkataba wake wa miaka miwili uliotakiwa kuisha Julai mwaka huu umechezewa na kuonyesha unaisha Julai mwakani.
Uongozi wa Simba kwa mara kadhaa umepinga suala hilo ukidai Messi aliongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi alipoboreshewa maslahi yake mwaka juzi, jambo ambalo limepingwa vikali na winga huyo.
Katibu Msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala, ameliambia MTANZANIA jana kuwa wameshamaliza kushughulikia malalamiko ya Messi kuhusu utata wa mkataba wake, huku akidai kati ya leo au kesho watalifikisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.
“Tunaandaa taratibu za kulipeleka hili suala TFF kwenye Kamati ya Hadhi za Wachezaji kwa sababu tulichobaini sisi ni kweli huyu mtoto hakusaini mkataba wa miaka mitatu, alisaini mkataba wa miaka miwili, lakini kuna baadhi ya vitu vimefanyika kinyume na utaratibu.”
“Kwa hiyo tumekusanya evidence (ushahidi) kuhusu hilo suala na tunalipeleka kwenye Kamati hiyo ya Hadhi za Wachezaji ili wao waone hilo lina ukweli upi. Lakini sisi kwa sasa hatuwezi kusema kuwa mkataba ule ni feki au umeghushiwa kwani vyombo vya usalama pekee ndivyo vinaweza kubaini suala hilo,” alisema.
Kasabalala aliongeza kuwa mkataba wa miaka miwili aliosaini staa huyo Julai mwaka juzi ulikuwa na saini ya Katibu Mkuu wa zamani wa timu hiyo, Evodius Mtawala na Kaimu wa Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Kinesi’.
“Hakuongeza mkataba wa mwaka mmoja kama inavyodaiwa wakati anaongezewa maslahi ulipoingia uongozi mpya na mkataba huo wenye utata umesainiwa na Evans Aveva (Rais) na Kaburu (Makamu wa Rais),” alisema.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Aveva na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao ziliita bila kupokelewa.
Hata hivyo, Hanspope alifanya mahojiano maalumu na gazeti hili juzi jioni na kusema kuwa wamepanga kumshtaki Messi kama ataendelea kuichafua klabu hiyo kwenye vyombo vya habari.
“Sisi tumeshampa masharti yetu kumaliza suala hilo, atuletee mkataba original (halisi), lakini bado hajafanya hivyo anabaki kuongea na vyombo vya habari kama ndivyo vitamsaidia, tunachofikia baadaye hali hiyo ikizidi tutamshtaki kwenye vyombo husika,” alisema.
Simba katika kuimarisha kikosi chao wamewaongeza wachezaji watano mpaka sasa ambao ni kiungo, Peter Mwalyanzi (Mbeya City), kipa Mohamed Abraham Mohamed (JKU), mabeki Mohamed Faki (JKT Ruvu) na Samih Haji Nuhu na mshambuliaji wao wa zamani, Mussa Hassan Mgosi (Mtibwa Sugar), huku ikiwa katika mazungumzo ya mwisho na mshambuliaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles