31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Simba bado haijalipa deni la Musoti

Donald Musoti
Donald Musoti

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

LICHA ya tishio la kushushwa daraja lililotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa Simba, uongozi wa klabu hiyo hadi sasa bado haujaonesha nia ya dhati ya kulipa deni la shilingi milioni 73 la mchezaji Mkenya, Donald Musoti, kama ilivyotakiwa kufanya hivyo.

Deni hilo lililotokana na Simba kupuuza kumlipa mchezaji huyo baada ya kuvunja mkataba wake aliposajiliwa msimu wa 2014/15, kitendo ambacho kilimfanya Musoti kukimbiza malalamiko yake Fifa ambao waliona mchezaji huyo ana hoja.

Mei 6 mwaka huu, Fifa iliitaka TFF kusimamia malipo ya deni hilo na kuhakikisha Simba inalipa ndani ya siku 30 hadi kufikia Juni 6 mwaka huu, lakini bado klabu hiyo haijafanya hivyo.

Chanzo cha uhakika ndani ya TFF kililieleza MTANZANIA jana kwamba bado hawajapokea stakabadhi yoyote ya malipo na hawana taarifa juu ya malipo hayo kama yalifanyika.

“Tumefanya mawasiliano na Shirikisho la Kenya pia Fifa juu ya malipo ya deni hilo na hakuna taarifa ya Simba kulipa.

“Simba walidai wangelipa deni hilo hadi watakapolipwa deni la milioni 600 la mauzo ya mchezaji wao, Emmanuel Okwi, aliyesajiliwa na timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

“Tayari deni la Okwi walishalipwa lakini wanalodaiwa na Musoti hawajalipa  hadi sasa, kwani wangelipa lazima tungejua kwa kuwa sisi ndio wasimamizi wa malipo ya deni hilo,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa  kutokana na kuendelea kupuuzia malipo hayo huenda Fifa ikatekeleza agizo lake la kuishusha timu hiyo daraja.

“Kuna ujanja mwingi unaendelea katika malipo ya deni hili na kama Simba wasipokuwa makini wanaweza kushuhudia timu yao inashushwa daraja kwa kosa hili,” kilisema chanzo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles