25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA SC MSAKO WAHAMIA KAGERA SUGAR

NA ZAITUNI KIBWANA 

USHINDI wa mabao 2-1 ilioupata Simba juzi dhidi ya Coastal Union, umempa mzuka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems ambaye amesema kamatakamata yao ya pointi tatu itaendelea hadi mwisho wa msimu.

Simba iliibuka na ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Wekundu hao tangu walipotupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa katika hatua ya robo  fainali.

Kikosi cha Simba sasa kinajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems alisema vijana wake wamekomaa kiasi cha kutosha katika kuipigania timu yao na kupata ushindi katika michezo yao ukiwemo dhidi ya Kagera Sugar.

“Najua utakuwa mchezo mgumu lakini sisi tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu, tunachohitaji ni kutetea ubingwa wetu.

 “Timu yoyote inapoanza msimu wa ligi inapaswa kuwa na malengo, sisi Simba msimu huu tulipanga kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa, kufanya vema Kombe la Azam, Sport Pesa lakini hatukufanikiwa, tumebaki na lengo la ubingwa wa Ligi Kuu,” alisema.

Kocha huyo kipenzi cha mashabiki Simba, alisema kutokana na ugumu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa, ameamua kutotaka mzaha katika michezo  yao kwa kuongeza umakini ili kuhakikisha wanashinda michezo yao yote.

 “Nimewaambia wachezaji wangu tunahitaji kushinda michezo yetu yote ili kutimiza malengo yetu na  hatutawadharau wapinzani, tutapambana hadi hatua ya mwisho,” alisema.

Wakati Aussems akiyasema hayo, Mratibu wa timu hiyo, Abasi Ally, alisema timu hiyo itaondoka Dar es Salaam alfajiri ya leo ikiwa na kikosi kamili.

 “Wachezaji wote watakwenda Mwanza, hakuna atakayebaki, tunaondoka na ndege na tukifika jioni tutafanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo,” alisema.

Wekundu hao wa Msimbazi kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kufikisha pointi 60 kupitia mechi 23, wakiwa nyuma ya Azam FC yenye pointi 66 kupitia mechi 31 na vinara Yanga wenye pointi 74, baada ya kucheza mechi 32. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles