28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Sido yatoa mafunzo ya ubanguaji korosho kwa wajasiriamali

Hadija Omary, Lindi

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) Mkoa wa Lindi limewapatia mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho wajasiriamali 48 kutoka Wilaya za Lindi na Nachingwea mkoani humo.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza kasi ya uongezaji wa thamani katika zao la korosho ili wananchi waweze kupata kipato kupitia ubanguaji na kutoa ajira katika jamii.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo Ofisa Uendelezaji Mafunzo wa shirika hilo Isack Daniel, amesema katika mafunzo hayo ya siku tano washiriki wamepata fursa ya kujifunza hatua za ubanguaji bora wa korosho, teknolojia na ubanguaji bora wa korosho, usalama na afya kiwandani.

Aliyataja mambo mengine waliyojifunza ni ubora, usalama na usafi wa chakula (korosho) katika uzalishaji, utumiaji na matengenezo madogo madogo katika mashine za ubanguaji, upangaji wa madaraja, ufungashaji na utunzaji wa madaraja kwa korosho zilizobanguliwa.

Kwa upande wake Meneja wa Sido Mkoa wa Lindi, Mwita Kasisi, amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa endelevu katika wilaya nyingine na yatafanyika kwa kuzingatia mahitaji ya wilaya husika.

“Baada ya mafunzo hayo washiriki wataweza kupata ajira kutokana na viwanda vya ubanguaji wa korosho vitakavyofunguliwa  na wengine watakwenda kuanzisha viwanda vyao ambavyo vitatengeneza ajira kwa wananchi wengine,” amesema.

Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga, aliwataka wajasiriamali wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya ubanguaji  wa korosho iliyotolewa na serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wabanguaji wadogo Mkoa wa Lindi,  Mwalimu mstaafu Mariamu Kaisi, amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi tofauti na awali walipokuwa  wanabangua korosho hizo kwa mazoea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles