31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Sido yajipanga kukabiliana na katazo la mifuko ya plastiki

Derick Milton, Simiyu

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji, amesema wamejipanga kutoa mafunzo kwa wajasiriamali nchi nzima jinsi ya kutengeneza mifuko mbadala baada ya ile plastiki kuzuiwa.

Profesa Mpanduji ameyasema hayo leo Jumatano Mei 29, wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Sido Mkoa wa Simiyu na mkandarasi Suma JKT baada ya kukamilisha ujenzi wake yaliyofanyika mjini Bariadi.

Amesema katika kuelekea kuanza kwa utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, shirika hilo litahakikisha wanatoa fursa kwa kila mjasiriamali kujifunza namna ya kutengeneza mifukohiyo.

“Kwa sasa tumeanza Mkoa wa Dar es Salaam kutoa mafunzo na baadaye tutaendelea kutoa mafunzo hayo kwa mikoa mingine ambayo ina ofisi za Sido.

“Kwa sasa watafundishwa kutengeneza kwa kutumia mikono huku tukisubiri mashine,” Profesa Mpanduji.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi hiyo meneja wa Suma JKT kanda ya Ziwa, Luteni Kanali Petro Ngata, ameishukuru Sido kwa kuwaamini na kuwapatia zabuni ya ujenzi wa ofisi huo ambao umekamilika kwa asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles