25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE BINAFSI ZATAKIWA KUWARUDISHA WANAFUNZI WALIOKOSA WASTANI WA KUFAULU

NA AZIZA MASOUD- DAR ES SALAAM

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeziagiza shule zote binafsi zilizowakaririsha au kuwafukuza wanafunzi kwa kigezo cha wastani wa ufaulu kuwarudisha shuleni ifikapo Januari 20, mwaka huu ili waendelee na masomo.

Pia wizara imetishia kuwafungia na kuwafutia usajili wamiliki wote wa shule watakaokaidi agizo hilo ambalo uamuzi wake umeenda kinyume na Waraka wa Elimu namba saba wa mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Kamishna wa Elimu wa wizara hiyo, Dk. Edicome Shirima, waraka wa elimu umepiga marufuku utaratibu wa shule zisizo za Serikali kukaririsha darasa, kufukuza au kuhamisha mwanafunzi aliyefanya na kufaulu mtihani wa darasa la nne, kidato cha pili na cha nne kwa kigezo cha kutokufikia wastani wa ufaulu wa shule husika.

Shirima alisema pamoja na kutolewa kwa waraka huo, hivi karibuni wizara hiyo imebaini kuwapo kwa baadhi ya shule zisizo za Serikali kukaririsha na kuhamisha wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu wa shule.

“Baadhi ya wakuu wa shule wamefikia hatua ya kuwatuhumu wanafunzi kuwa na makosa ya utovu wa nidhamu na kisha kuwaeleza wazazi au walezi wa wanafunzi husika kuwa adhabu ni kurudia darasa au kuwarejesha shuleni kwa masharti ya kuwatafutia shule ama vituo vingine vya kufanyia mitihani yao ya mwisho.

“Jambo hili ni kinyume na taratibu za sheria, miongozo na taratibu zilizowekwa na wizara, kutokana na ukiukwaji huo wa taratibu zilizowekwa na wizara, kuanzia leo (jana Januari 12, mwaka huu), wizara inaziagiza shule zote zilizokaririsha au kufukuza shule wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu wa shule kuwarejesha shuleni wanafunzi hao ifikapo Januari 20, mwaka huu ili waendelee na masomo,” alisema.

Shirima alisema wanafunzi hao watakaporudishwa shuleni wanapaswa kuendelea na masomo katika madarasa  yao wanayopaswa kuwapo kisheria na wahusika wahakikishe wanaandikishwa kufanyia mitihani yao ya mwisho katika shule hizo na si vituo.

Pia aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wote ambao watoto wao walirudishwa nyumbani kuwapeleka shuleni wanafunzi katika muda uliotajwa na wizara ili waendelee na masomo.

“Shule ambayo itakaidi agizo hili wizara itawachukulia hatua za kisheria ikiwamo kufungiwa usajili wa wanafunzi na kufutiwa usajili wa shule,” alisema. Inaendelea………

Kwa habari zaidi usikose nakala yako.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles