30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SHIRIKISHO LATAKA HATUA KALI KUKABILI DAWA ZA KULEVYA

NA OSCAR ASSENGA

SHIRIKISHO  la Vyuo vya Elimu ya Juu mkoani Tanga limeitaka serikali iwachukulie hatua kali watu waliotajwa kujihusisha na matumizi ya  dawa za kulevya   iwapo watabainika kutumia.

Limesema ni muhimu pia kuwabana wafanyabiashara wa dawa hizo kuweza kuumaliza mtandao huo.

Shirikisho hilo pia limeunga mkono juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda la kupambana na watumiaji wa  dawa za kulevya mkoani humo.

Limewataka wakuu wa mikoa mengine kuunga mkono suala hilo.

Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mkoani Tanga, Justus Gration alikuwa akizungumzia  hatua ya  Makonda kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.

 Alisema suala la utumiaji wa dawa za kulevya haliwezi kumalizika iwapo watanzania hawatakuwa na ushirikiana wa dhati kwenye mapambano hayo kwa kuwafichua wahusika.

Gration alisema hatua hiyo itaiwezesha  jamii  kuepukana na tatizo hilo.

“Kimsingi naunga mkono jitihada za serikali kupambana na kutokomeza dawa za kulevya.

“Kwa moyo wa dhati kabisa nampongeza RC Makonda kwa juhudi anazozichukua lakini pia watanzania tuendelee kumpa ushirikiana  kuendelea kufichua magenge makubwa  yanayohusika.

“Lakini vita ya dawa za kuveya isiishie mkoani Dar es Salaam pekee bali yawe ni mapambano nchi nzima.

“Jambo hilo limeathiri vijana wengi na kama likifika mkoani Tanga mimi nitakuwa tayari kuunga mkono,” alisema

Aliwataka vijana shuleni kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa kuwafichua baadhi yao ambao wanajuhusisha na matumizi hayo.

“Nisisitize tu endapo wanaotajwa kutumia dawa aa kulevya au kuziingiza nchini wakikutwa na hatia nashauri serikali iwachukulie hatua kali na nzito ili kuutokomeza mtandao huo ambao ni hatari kwa maendeleo,“ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles