Imechapishwa: Thu, Jun 7th, 2018

Shilole: Nakwenda kumzika mzazi mwezangu

Na LULU RINGO


MSANII wa muziki na filamu nchini Zuwena Mohammed (Shilole) amesema atakwenda Igunga mkoani Tabora kumzika mzazi mwenzake, Makala Elia waliofanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike (Joyce).

Akizungumza na Mtanzania Digital kwa masikitiko Shilole alisema amepokea taarifa za msiba za mzazi mwenzake huyo kwa mshtuko mkubwa na sasa amemuachia kumbukumbu ya mtoto wa kwanza kati ya wawili alionao.

“Natarajia kwenda kushiriki katika mazishi yatakayofanyika Igunga na Marehemu nimezaa nae mtoto wangu wa kwanza wa kike Joyce,” alisema.

Shiloe na Marehemu makala waliwahi kuishi pamoja kama mume na mke kabla ya msanii huyo kuhamia jijini Dar es Salaam ambako anaishi na mume wake waliyefunga ndoa miezi kadhaa iliyopita.

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

Shilole: Nakwenda kumzika mzazi mwezangu