SHERIA MPYA KUWASAIDIA  WANAWAKE NCHINI MOROCCO

0
453

Morocco


Sheria mpya ya kupambana na unyanyasaji wa kingono na udhalilishaji wa mwanamke nchini Morocco, itaanza kutekelezwa hivi karibuni.

Sheria hiyo ambayo inafanya suala hilo lionekane ni uhalifu inajumuisha upigaji marufuku wa ndoa za kulazimishwa.

Sheria hiyo imefikiwa kutokana na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni juu ya kiwango cha udhalilishaji wanawake.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa la kudhalilisha kingono hadharani iwe kwa kutumia maneno au ishara yoyote ya kudhalilisha kijinsia atakabiliwa na hukumu ya kifungo kuanzia mwezi mmoja mpaka sita gerezani na faini ya fedha taslimu.

Sheria hiyo mpya imepokelewa vizuri lakini pia imekosolewa kwa sababu haifafanui vizuri juu ya unyanyasaji huo majumbani na vitendo vya ubakaji ndani ya ndoa.

Shirika la haki za binadamu inasema kuwa wanawake wengi nchini Morocco, wamekuwa waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kingono.

Katika ripoti yake ya mwaka 2015, Shirika la Haki za Binadamu nchini humo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 20 ya wanawake nchini Morocco, wamekumbwa na matukio ya unyanyasaji wa kingono japo mara moja katika maisha yao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here