26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sheria hairuhusu polisi kupiga mtuhumiwa

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

BUNGE limeelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 11, kinaelekeza askari polisi hatakiwi kumpiga au kumtesa mtuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati akiwa mikononi mwa Polisi au kwenye kituo cha Polisi.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Chonga, Mohamed Juma Khatibu (CUF).

Khatibu alihoji ni katika mazingira gani askari anapaswa au kulazimika kumtesa mtuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati akiwa mikononi mwake au kituo cha polisi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, alisema kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 11 kinaelekeza namna ya ukamataji.

Masauni alisema kifungu hicho mahususi cha ukamataji hakimruhusu askari kumpiga au kumtesa mtuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati akiwa mikononi mwa Polisi au kwenye kituo cha Polisi.

“Kanuni za kudumu za utendaji wa Jeshi la Polisi (PGO), zinakataza na kuelekeza utendaji kazi wa askari polisi ambapo askari yeyote anapobainika kufanya vitendo vya kumpiga au kumtesa mtuhumiwa huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani,” alisema Naibu Waziri Masauni. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles