27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Shein kufungua mkutano wa maafa

Ramadhan Hassan-Dodoma

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kwanza wa kamati ya mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajia kuanza kesho hadi Februari 21,  mwaka huu.

Akizungumza mwishoni mwa wiki  waandishi wa habari jijini Dodoma,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama alisema mkutano utajidili masuala mbalimbali.

“Kufanyika  mkutano huu kwetu, ni fursa kubwa kwa wananchi wa Tanzania,utasaidia kukuza biashara na utalii katika nchi yetu hasa visiwa vya Zanzibar na kuendelea kujitangaza kimataifa,”alisema.

Alisema kamati ya mawaziri wenye dhamana ya menejimenti ya maafa, imeanzishwa kwa lengo la kulishauri baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kuhusu masuala ya upunguzaji wa madhara ya maafa kikanda.

Alisema  lengo mahususi pia ni kuwa na jukwaa la kubadilishana taarifa na uzoefu wa kiutendaji miongoni mwa nchi wanachama ili kutekeleza kwa ufanisi shughuli za usimamizi wa maafa.

“Mkutano huu unakuja kipindi ambacho nchi nyingi wanachama,zimekuwa zikiathiriwa na majanga ya asili mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa.

“Tunakumbuka ukame wa mwaka 2016 ambao uliathiri takribani watu milioni 40 katika ukanda huu na kusababisha ukosefu wa chakula. Idadi hii iliongezeka hadi watu milioni 41.6 katika nchi 13 wanachama kipindi cha msimu wa 2018/19,”alisema.

Majanga hayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa, yamekuwa yakitokea magonjwa ya milipuko ya wanyama na mazao.

“Hali hii imekuwa ikichangia kudumaza ukuaji wa uchumi wa kikanda, hatuna budi kuchukua hatua kwa pamoja za kupunguza madhara, kuimarisha utayari wa kikanda na uwezo wa kukabiliana na maafa,”alisema.

Katika kuchukua hatua za kuimarisha ustahimilivu wa kikanda dhidi ya maafa, sekretarieti ya jumuiya kwa kushirikiana na nchi wanachama, imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuimarisha ustahimilivu kwa kuandaa mpango wa dharura wa kujiandaa na kukabiliana na Maafa.

“Lengo kubwa  ni kuhakikisha kila sekta inazingatia hatua za upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango ya maendeleo na uandaaji wa bajeti ili kupunguza madhara kwa jamii na hasara za kiuchumi,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles