25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SHEIN AIPA MAELEKEZO WIZARA YA AFYA

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameutaka uongozi wa Wizara ya Afya kuwafahamisha wananchi juu ya mikakati iliyowekwa na Serikali  kuhakikisha   dawa zinapatikana katika hospitali za Serikali Unguja na Pemba.

Agizo hilo alilitoa jana alipokutana na uongozi wa Wizara ya Afya   ulipowasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2016/17, Mpango kazi kwa bajeti ya mwaka 2017/18 na utekelezaji wake kwa  kipindi cha robo ya kwanza.

Licha ya hali hiyo, alipongeza uongozi wa wizara hiyo kuhusu taarifa ya hali ya upatikanaji wa dawa za maradhi mbalimbali Zanzibar kuwa imeimarika.

“Kuna haja ya kuwajuilisha na kuwaelimisha wananchi juu ya kuwapo aina mbalimbali za dawa na vigezo vinavyozingatiwa katika kuzitoa kuepuka manung’uniko kutoka kwa wananchi,” alisema.

Dk. Shein aliupongeza uongozi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Afya na kueleza haja kwa wizara hiyo kuendelea kusimamia vema huduma za afya kwa wananchi  na kuendelea kutoa elimu ya afya kwa jamii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd naye alihudhuria kikao hicho.

Dk. Shein pia  alisifu hatua iliyofikiwa katika kujitolea kutoa damu na kuwapongeza wananchi kwa jinsi wanavyojitokeza kwa wingi kutoa damu.

Alitilia mkazo katika kutoa mafunzo ya huduma za meno kwa kuzingatia kwamba hadi sasa Zanzibar wapo wataalamu wachache katika fani hiyo.

Dk. Shein alisema itakuwa ni vema ikiwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kitaanza kutoa mafunzo hayo pamoja na Wizara ya Afya kupeleka wanafunzi nje ya nchi kusomea fani hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles