24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Sharapova abainika kutumia madawa

Maria SharapovaCANBERRA, AUSTRALIA

NYOTA namba moja wa zamani katika mchezo wa tenisi, Maria Sharapova, amethibitisha kubainika kwamba alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika michuano ya wazi ya Australia mwaka huu.

Sharapova ambaye ni raia wa nchini Urusi, mwenye umri wa miaka 28, amepimwa na kubainika kutumia dawa aina ya Meldonium, ambazo amekua akitumia toka mwaka 2006.

Mcheza tenisi huyu mshindi wa Grand Slam mara tano, alisema hakujua vikwazo atakavyokuja kukutana navyo baadaye.

“Kwa miaka 10 nimekua nikitumia dawa zinazoitwa Mildronate nikipewa na daktari wangu na familia yangu.

“Siku chache zilizopita nilipokea barua kutoka kwa Shirikisho la Tenisi la Kimataifa (ITF), juu ya dawa hizo na nikagundua kuwa zina jina jingine la Meldonium.

“Ni muhimu sana kuelewa kwa miaka 10 dawa hizo hazikua kwenye orodha ya shirika la kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Wada), lakini sheria zilibadilika January na kuzifanya dawa za Meldonium kukatazwa, kitu ambacho sikufahamu. Desemba mwaka jana nilipata barua pepe toka Wada kuhusu mabadiliko kwa dawa zilizokatazwa, ila sikufungua barua hiyo na ndiyo maana yamenikuta haya,” alisema Sharapova.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles