24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Shangwe zaibuka baada ya Kim Jong Un kutokea hadharani

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

BAADA ya minong’ono mingi kuhusu afya yake, wengine wakienda mbali na kusema amekufa, hatimaye chombo cha habari cha serikali  kimetoa picha ya kiongozi anayetajwa kuwa mtata  wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ikimwonyesha anafungua kiwanda cha mbolea juzi Ijumaa.

Chombo hicho cha Serikali kimesema Kim Jong ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani  baada ya siku 20.

Shirika la habari la KCNA limeripoti kwamba Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini katika ufunguzi huo wa kiwanda cha mbolea alikata utepe.

Shirika hilo la habari liliongeza kuwa watu waliokuwapo katika kiwanda hicho walilipuka kwa shangwe baada ya Kim Jong Un kuonekana kiwandani hapo.

Taarifa za kuonekana kwake hadharani zimekuja baada ya mara ya mwisho  kuonekana katika shughuli za kiserikali Aprili 12 mwaka huu huku ikizuka minong’ono kuhusu afya yake.

Shirika la habari la Uingereza la BBC limesema taarifa hizo mpya kutoka katika chombo cha habari cha Korea Kaskazini haziwezi kuwa za mwisho au huru kuthibitisha kuonekana kwa kiongozi huyo.

Chombo hicho cha habari cha Serikali baadae kilitoa picha kadhaa kikisema zinamuonyesha Kim akikata utepe nje ya kiwanda hicho.

Alipoulizwa kuhusu kuripotiwa kuonekana kwa Kim hadharani, Rais wa Marekani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakutaka kuzungumza chochote.

KILICHOSEMWA NA CHOMBO CHA HABARI CHA SERIKALI 

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha serikali cha nchini Korea Kaskazini, Korean Central News Agency (KCNA), katika ufunguzi huo wa kiwanda cha mbolea, Kim alikuwa ameongozana na maofisa kadhaa waandamizi  wa Korea Kaskazini, akiwamo dada yake Kim Yo Jong.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alikata utepe kuashirika uzinduzi wa kiwanda hicho katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo katika eneo la Kaskazini Pyongyang.

“Watu waliohudhuria hafla hiyo walilipuka kwa shangwe; ‘hurrah!’  kwa kiongozi huyo wa juu ambaye anaongoza watu wote na kusimamia ustawi wa taifa “, lilieleza KCNA katika taarifa yake.

Kim alieleza kufurahishwa na mfumo wa uzalishaji wa kiwanda hicho, na kukipongeza kwa kuchangia maendeleo ya nchi hiyo husuani katika viwanda vya kemikali na uzalishaji wa chakula, liliongeza shirika hilo la habari.

Tetesi kuhusu afya ya Kim zilianza kuenea baada ya kutoonekana katika shehere za maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake, mwasisi wa taifa hilo Kim Il Sung  Aprili 15  mwaka huu.

Maadhimisho hayo ni moja katika shehere kubwa katika kalenda ya Korea Kaskazini, na kwa kawaida Kim amekuwa akiadhimisha kwa kutembelea eneo ambalo babu yake huyo amezikwa. Kim hajawahi kukosa shughuli hiyo.

Madai juu ya afya mbaya ya Kim kisha yalipatikana katika ripoti ya tovuti inayoendeshwa na wakosoaji wa  Korea Kaskazini.

Chanzo ambacho kilifichwa kililidokeza Daily NK kwamba wanafahamu Kim alikuwa akipambana na tatizo la moyo tangu Agosti mwaka jana “lakini hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kutembelea mara kwa mara huko katika mlima  Paektu.

Taarifa hizo kutoka katika chanzo kimoja ndizo zilizosambaa katika vyombo vya habari vya kimataifa.

Mashirika ya habari yalianza kuripoti madai hayo, hadi pale zilipoibuka taarifa kuwa mashirika ya kijasusi ya Korea Kusini na Marekani zinafuatilia madai hayo.

Baada ya hapo vikaibuka vichwa vya habari cha kushtua kwenye vyombo vya habari vya Marekani  kwamba kiongozi huy wa Korea Kaskazini alikuwa katika hali mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo naye alionekana kuongeza mafuta kwenye moto kuhusu tetesi hizo Aprili 29, kwa kusema maofisa wa Marekani hawajamuona Kim hivi karibuni.

Ingawa taarifa kutoka katika Serikali ya Korea Kusini, na vyanzo kutoka ndani ya vyombo vya usalama vya China  vilivyozungumza na Shirika la habari la Reuters – vilisema taarifa hizo si sahihi.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa Kim kupotea hadharani, Septemba 2014 hakuonekana kwa siku 40 baada ya kuhudhuria tamasha na alikuja kuonekana katikati ya mwezi Oktoba akitumia fimbo.

Chombo cha Serikali hakikufafanua alikuwa wapi.

Lakini Shirika la Kijasusi la Korea Kusini lilisema huenda wakati huo alifanyiwa upasuaji  mguuni katika eneo la ‘ankle’ kutokana na tatizo maumivu.

UCHAMBUZI WA MWANDISHI

Katika uchambuzi wake kuhusu jambo hilo, Mwandishi wa BBC, Laura Bicker aliyeko Korea Kusini anasema; Tahadhari mara nyingi hutupwa kando wakati vyombo vingi vya habari vya kimataifa vinaporipoti juu ya Korea Kaskazini. Uchekeshaji mwingi, uvumi wa kudanganya unaweza kulisha tasnia inayojua kuwa vichwa vya vya habari vya kichochezi dhidi ya Kim Jong-un ni suala kubwa.

Kuripoti juu ya hali ya usiri ni ngumu. Ukweli na vyanzo ni ngumu sana kupata, hasa kwa kutokana na nchi  ya Korea Kaskazini kujifungia kwa sababu ya janga la Covid-19.

Hata Serikali ya Korea Kusini ni wazi kwamba haikugundua shughuli zisizo za kawaida za Kaskazini.

Mara nyingi Korea Kusini ina vyanzo vya kijasusi bora kabisa kutoka Korea Kaskazini.  Lakini pamoja na hayo huko nyuma hawakuwahi kuwa na taarifa sahihi.

Pengine tuweke wazi. Huenda Kim Jong-un alikuwa mgonjwa, au alifanyiwa upasuaji wiki mbili zilizopita. Au alikuwa varandani kwake karibu kabisa na boti yake nyumbani kwake Wonsan akicheka juu ya tetesi zilizokuwa zikizunguka duniani. Kutokuwepo kwake kwa siku 20 kunaweza kusiwe na msingi sana pia juu ya afya yake.

Bado kuna maswali halali ya kuulizwa kuhusu mrithi wake na ni mipango gani iliyopo ikiwa jambo litatokea kwake.

Lakini kuna jambo moja ambalo limepotea katika haya yote. Korea Kaskazini ni zaidi ya mtu mmoja. Ni nchi ya watu milioni 25 ambayo mara nyingi hupuuzwa.

Leo  hii kurejea tena kwa Kim katika kiwanda cha mbolea ukweli ni kwamba vichwa vya habari vitazingatia kurudi kwake, na si mahali alikokuwa au kama kiwanda alichokizindua iwapo kitasaidia nchi kukabiliana na uhaba sugu wa chakula.

Nakuhakikishia, kwamba kwa watu wa Korea Kaskazini hivi sasa, hilo ni muhimu kuliko kukosekana kwa kiongozi wao ambaye hakuelezewa alikokuwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles