33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawataka watafiti kuharakisha utafiti bomba la mafuta Tanga

Susan Uhinga, Handeni



Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,  amewataka wataalamu wanaofanya kazi za utafiti kwenye njia ya bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kazi hizo zikamilike Novemba mwaka huu.

Dk. Kalemani ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 7, baada ya kutembelea moja ya eneo zinakofanyika shughuli hizo katika Kata ya Kiomoni wilayani Tanga na kukuta wataalamu wakiendelea na kazi hizo.

“Mnafanya kazi nzuri lakini lazima mhakikishe kuwa kazi hizi zinamalizika hadi kufikia Novemba mwaka huu ili Januari mwakani tuanze rasmi kazi ya ujenzi,” amesema Dk. Kalemani.

Awali, mwakilishi wa Serikali anayesimamia tafiti za jiotekniko kwenye njia ya bomba, Alphonce Kilovele, amesema kuwa tafiti hizo ni mwendelezo wa tafiti za kijiolojia na kijiofizikia ambazo zimekwishakamilika.

“Utafiti wa kijiotekniko unahusisha uchorongaji wa visima ili kupata sampuli za udongo, miamba na sampuli za maji kwa kwa ajili ya kuzipeleka maabara ili kufanyiwa upembuzi wa takwimu za kihandisi zitakazosaidia uboreshaji wa usanifu wa miundombinu ya njia ya bomba.

“Kazi hizi tunazofanya pia zitasaidia kazi za usanifu wa vituo vya kupashia na kusukuma mafuta ambavyo vitajengwa sambamba na ulazaji wa bomba la mafuta,” amesema Kilovele.

Kuhusu ushirikishwaji wa wazawa katika kazi hizo amesema kuna kampuni za Kitanzania zinazotoa huduma mbalimbali ikiwemo usafiri, utoaji wa wataalamu, matibabu, ulinzi na chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles