26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawasilisha hoja 10 mahakamani kuwapinga wapinzani

PATRICIA KIMELEMETA NA LEONARD MANG’OHA

SERIKALI imewasilisha hoja 10 kesi ya kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake.

Walalamikaji wengine katika kesi hiyo  ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Joran Bashange na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma (CUF), Salim Bimani.

Shauri hilo linasikilizwa na Jaji Benhajo Masoud, huku upande wa walalamikaji wakiwakilishwa na Wakili Mpare Mpoki na upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo.

Wakili Mulwambo alidai kuwa Katiba ya nchi imegawa mamlaka na kuyaheshimu.

Pia alidai kuwa mhimili wa Mahakama hauwezi kuingilia mhimili wa Bunge katika kujadiliana mambo yake.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa mahakama inaweza kujadili sheria iliyotungwa na Bunge na si muswada ambao haujapitishwa uwe sheria.

“Waombaji wamewasilisha maombi yao na kiapo chenye udhaifu bila ya kuwa na saini ya mlalamikaji wa kwanza (Zitto), jambo hilo pekee linasababisha shauri hilo kukosa nguvu ya kisheria na linapaswa kuondolewa mahakamani.

“Kwa sababu muswada sio sheria hadi usainiwe ndio uweze kuwa sheria, ninaiomba mahakama yako kwa sasa kuliacha Bunge lifanye kazi yake kisheria, hata hivyo muswada huo haupo katika Ofisi ya Waziri mkuu wala Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, muswada upo bungeni,” alidai Mulwambo.

Pia alidai kutokana na udhaifu huo, aliiomba mahakama hiyo kuliondoa shauri hilo mahakamani hapo.

Alidai wabunge wana uwezo wa kutoa maoni ya marekebisho bungeni kwa kuwawakilisha wananchi.

Hata hivyo, upande wa walalamikaji ukiongozwa na Wakili Mpoki, umetaka ibara ya 5 katika Katiba inayoipa mahakama mamlaka ya kukitengua kifungu hicho au kuchukua hatua yoyote dhidi ya Serikali au mamlaka yoyote kwa kukiuka haki, uhuru na wajibu kama ilivyoanisha ibara ya 12 hadi 29 katika Katiba ya nchi.

Hata hivyo, Jaji Masoud, aliahirisha shauri hilo hadi Januari 14, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles