30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yavunja mkataba na mkandarasi ujenzi wa stendi ya mabasi Bariadi

Derick Milton, Simiyu

Serikali imefikia uamuzi wa mwisho juu ya mkandarasi ambaye alikuwa akijenga stendi ya kisasa ya mabasi katika Halmashuari ya mji wa Bariadi kwa kuvunja mkataba kutokana na kubainika kuwa hawa uwezo wa kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Merkzedeck Humbe mbele za waandishi wa habari ambapo amesema kuwa mbali na ujenzi wa stendi mkandarasi huyo alikuwa akijenga pia barabara ya kilometa 1.5 inayozunguka stendi hiyo hadi Ikulu ndogo.

Humbe amesema kuwa mradi huo ambao unafadhiliwa na benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali unatekelezwa kwa kiasi cha Sh. Bilioni 7.2, ambapo mpaka wanavunja mkataba huo mkandarasi huyo amelipwa kiasi cha Sh. Bilioni 5.1.

“Kazi hii ilianza rasmi Novemba 3, 2017 na ilitakiwa kumalizika Novemba 3, mwaka huu lakini ameshindwa bila sababu za msingi, ameomba kuongezewa muda mara mbili tumemkubalia lakini bado ameshindwa, kama mwajiri nimepitia vifungu vyote vya sheria na taratibu zinazotakiwa na kuamua kuvunja mkataba, jana nimemwandikia barua ya kuvunja mkataba,” alisema Humbe.

Mratibu wa TARURA katika Halmashauri hiyo mhandisi Mathias Mugolozi alimtaja mkandarasi huyo kuwa ni Kings Builders na Halem Construction Co. Ltd kutoka Dar es salaam, ambapo aliandikiwa barua nyingi za onyo lakini bado kasi ya ujenzi imeendelea kuwa ndogo.

Mkuu wa Wilaya Festo Kiswaga amemtaka Mkurugenzi huyo ndani ya siku mbili kuhakikisha anatafutwa mkandarasi mwingine atakayekamilisha ujenzi huo na kufanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huo ukamilike Novemba 30, 22019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles