30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaunganisha Taasisi za mafunzo na wadau sekta ya utalii

Asha Bani

Serikali imesema taasisi za mafunzo na wadau wa sekta ya utalii wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamto zilizopo ikiwemo nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha katika tasnia hiyo. 

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha  wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la kuunganisha wanataaluma na wadau wa sekta ya Utalii na Ukarimu ambapo amesema ushindani katika soko ni mkubwa hivyo kunahitajika maandalizi mazuri ya rasilimali watu ili kuweza kushindana katika soko la dunia. 

Amesema utalii ni moja ya sekta inayolipatia  taifa fedha za kigeni akitolea mfano katika kipindi cha mwaka jana nchi ilipata fedha za kigeni Dola  milioni 2.4 kutokana na utalii na kusema kukiwa na nguvu kazi yenye weledi na ufanisi wa kutosha nchi itaneemeka kupitia sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha 

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kwa sasa Taifa linatoa kipaumbele katika kuimarisha viwanda ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuandaa nguvu kazi, hivyo ni vizuri kukawa na mfumo wa mafunzo pacha kati ya taasisi za mafunzo na wamiliki wa viwanda.

Naye Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Shogo Mlozi amesema kwa kushirikiana na vyuo vingine vinavyotoa mafunzo ya utalii wataendelea kuimarisha mpango wa utoaji mafunzo  kwa kufanya kazi karibu na watoa huduma ili kupata nguvu kazi yenye weledi na ujuzi.  

Kwa upande wake mshiriki wa kongamano hilo kutoka VETA makao makuu,  Happiness Salema amesema ni vizuri kukawa na makongamano ya aina hii kwa kuwa yanawaleta pamoja watoa mafunzo na wamiliki wa viwanda, jambo ambalo linasaidia kuona changamoto zilizopo na kuweka mkakati kwani nchi zilizoendelea zinatumia mfumo huu katika kutoa mafunzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles