26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa onyo kwa watorosha madini

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka watoroshaji wa madini hapa nchini kuacha tabia hiyo mara moja na kusisitiza anaendelea kufuatilia nyendo zao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, (DiTF), katika  Jukwaa la Madini Kuhusu Fursa na Changamoto katika Sekta ya Madini, alisema hawatamtumbia macho mtoroshaji wa madini atahakikisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Nitahakikisha sheria inafuata mkondo wake, ikibidi hata kuwataifisha madini yao,”alisema Nyongo

Alisema bado kuna utoroshaji wa madini lakini wanaendelea kupambana nap kwakuwa wanachangia kudidimiza uchumi wa nchi.

 Alisema madini mengi yamekuwa yakiendelea pia kupotea ardhini kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kisasa  hali inayosababishashirikiano wavjimbaji kutumia vifaa hafifu.

“Kuna sehemu nyingine dhahabu imechanganyikana na kopa kwa kuwa hatuna vifaa vya kisasa, tunashindwa kuvitoa kwa pamoja na kuchangia madini mengine kupotea,” alisema Nyongo.

Alisema masoko ya madini yamefikia 29, hivyo wachimbaji wayatumie kwa faida ya taifa na kuzuia utoroshaji.

“Nawaonya wanaouza madini kwa njia ya panya ole wao kwakuwa wakati umefika na mwisho wa biashara hiyo haramu ni sasa kwani watakiona cha moto,” alisema Nyongo.

Kutokana na vitendo hivyo, alitoa onyo kwa wanaoendesha kampeni ya kukamata watoroshaji hao kuacha kutekeleza agizo hilo kwa upendeleo.

Alisema Serikali inahitaji fedha kutoka sekta ya madini, hata mvumilia yeyote anayetumia mwanya huo wa madini kukinufaisha.

Alisema lengo la ni kukusanya Sh bilioni 470 ambapo hapo  awali walikusanya Sh bilioni 328.

Aliwashauri wafanyakazi wawe waaminifu wafanyekazi kazi kwa uadilifu na kuacha kushirikishwa vitendo hivyo viovu.

“Hadi sasa bado idadi kamili ya waliokamatwa hatujaipata lakini wengi kila siku wanakamatwa wakiwamo wafanyakazi wetu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa,” alisema Nyongo.

Pia aliigiza wawekezaji wa migodi kutoka nje ya nchi kujenga mazoea ya kununua bidhaa za ndani kwakuwa Kuna bidhaa za kutosha.

“Wapo wawekezaji ambao wanaendelea kununua bidhaa nje ya nchi naomba waache hiyo tabia haraka iwezekanavyo,” alisema Nyongo.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wenye Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uchimbaji wao bado ni hafifu hivyo ni muhimu kushirikishwa na wahimbaji was nje na kupata ujuzi.

Alisema wanaiomba Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE ikae na wachimbaji wadogo ili wake mahitaji yao kwani ukiwekeza kwenye madini inaweza kuchangia pato kubwa la Serikali.

Mwakilishi Shirika la Serikali linalosimamia Madini (Stamico), Joseph Samuyo alisema, wanaendelea kufanya utafiti ili kusaidia na wachimbaji wadogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles