25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa kibali dawa ya kutibu ini

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


SERIKALI imetoa kibali cha kuuza na kusambaza dawa ya figo na homa ya ini ya ijulikanyo   Billyd Fomula Power na Vission -2, iliyotengenezwa na mitishamba.

Dawa hiyo intarajiwa kusambazwa nchini katika maduka madogo na makubwa.

Mtafiti wa dawa hizo,  Danny Njau, alisema Dar es Salaam jana kuwa anaishukuru serikali kwa vile  amekua  akiifanyia utafiti kwa zaidi ya miaka 20 na sasa itasambazwa katika maduka madogo na makubwa.

Njau alisema tayari amepata vibali vyote kutoka Mamlaka Chakula na Dawa Tanzania  (TFDA), Mkemia Mkuu, Wizara Afya na watafiti wa masuala ya mimea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Sslaam.

Alisema amekwisha  kuthibitishwa kuanza shughuli hizo na Wizara ya Afya , Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kibali namba TZ 17 TM 0012,  tayari kwa kuanza kufanya kazi .

“Dawa hizi ni nzuri na watu watapona, nashukuru serikali kwa kunipatia kibali na sasa nitaanza usambazaji wa maduka madogo na makubwa.

“Lengo ni  kuwaponya watanzania wasiweze kuhangaika kwenda nje ya nchi kutafuta tiba wakati suluhisho lipo hapa hapa nchini.

“Kiwanda changu kipo Moshi kikubwa na tayari kimeanza kazi.

“Nimekuwa nikingoja kibali cha kuanza kusambaza tu…dawa hizi zitakuwa suluhisho kubwa kwa magonjwa hayo ambayo kwa sasa yameshika kasi kutokana na kutumia dawa zisizofaa na sababu za mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Njau.

Alisema Billyd Fomula Power ni dawa ya mitishamba iliyofanyiwa uchunguzi kwa miaka 20 na kuonyesha mafanikio makubwa kwa kutibu maelfu ya watu kwa muda mfupi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles