Serikali yasitisha sheria ya vipimo

0
2077

Arodia Peter, Dodoma

Serikali imesitisha kwa muda matumizi ya sheria ya vipimo inayotaka kutumia vifungashio katika usafirishaji wa viazi mviringo kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda sokoni.

Akisoma hotuba ya bajeti wa Wizara Viwanda na Biashara, bungeni leo Mei 14, waziri mwenye dhamana, Joseph Kakunda amesema sheria ilikuwa ikiwataka wazalishaji kutumia vifungashio maalum ambavyo kwa bahati mbaya upatikanaji wake una matatizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here