31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yashauriwa kutenga fedha nyingi za maendeleo

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
SERIKALI imeshauriwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha za bajeti yake katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ushauri huo ulitolewa Dar es Salaam jana na wadau wa maendeleo walioshiriki katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Policy Forum, uliojadili iwapo fedha zilizotengwa katika sekta ya elimu na afya ya uzazi zinakidhi.
Akizungumza katika mdahalo huo, Ofisa Utafiti na Uchambuzi na Sera wa HakiElimu, Makumba Mwenezi, alisema licha ya Serikali kutenga Sh trilioni 3.8 katika sekta ya elimu, lakini Sh trilioni 3.2 zimepelekwa katika mambo ya kawaida, huku Sh bilioni 600 pekee zikiwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
“Tunawekeza kiasi kikubwa cha fedha katika mambo ya kawaida na hata kile kidogo tunachowekeza kwa ajili ya miradi ya maendeleo tunakipeleka katika elimu ya juu, kwa kuwapatia mikopo wanafunzi, lakini tunajisahau kuwekeza katika ngazi ya msingi na sekondari ambako ndipo panapohitaji nguvu kubwa ya uwekezaji,” alisema Mwenezi.
Alisema sekta ya elimu imekuwa inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuwa chini ya idara nyingi za Serikali, jambo linalosababisha kutokuwapo kwa uwazi wa matumizi ya fedha hizo zinazotengwa.
“Ipo chini ya Tamisemi pamoja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, tuieweke chini ya idara moja ili fedha inapotengwa tujue kiasi chake na jinsi kitakavyotumika na hii itaondoa mianya ya ufujaji wa fedha na kila mara ripoti ya CAG inaonyesha udhaifu huo,” alisema Mwenezi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (UNA), Robert Kasenene, alisema Serikali inapaswa kuwekeza zaidi katika utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango na kuongeza wataalamu wa kutoa huduma na si dawa peke yake.
“Hivi karibuni Wizara ya Afya itawasilisha bajeti yake, inabidi ihakikishe inalifanyia kazi jambo hili kwa sababu tunahitaji kutoa elimu zaidi juu ya jambo hili,” alisema Kasenene.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles