27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAKIRI ONGEZEKO LA UHALIFU KWA BODABODA

 

 

Na Ramadhani Hassan, Dodoma

SERIKALI imekiri limekuwapo ongezeko la uhalifu  unaofanywa na waendesha bodaboda  katika maeneo mengi ya  Dar es Salaam.

Hayo yalielezwa   bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Subira Mwaifunga (Chadema).

Mwaifunga alisema  limekuwapo  wimbi kubwa la uhalifu unaofanywa na baadhi ya madereva bodaboda na bajaji katika maeneo mengi ya  Dar es Salaam.

‘’Je Serikali mpaka sasa imechukua hatua gani kudhibiti wimbi hili linalokuwa tishio kwa watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri.

‘’Je Serikali ina utaratibu gani wa kuhakiki na kutambua mmiliki, dereva na mahali zinaegesha  bajaji na bodaboda?’’aliuliza Mwaifunga.

Akijibu swali hilo, Mwigulu alikiri na kudai kuwa limekuwapo  ongezeko la uhalifu unaofanywa na waendesha bodaboda na bajaji katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Hata hivyo, Mwigulu alisema Serikali kupitia polisi  imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kama vile kufanya doria za magari, pikipiki na miguu  na kuanzisha na kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama  kubaini na kuzuia uhalifu.

Alisema Serikali kupitia Serikali za Mitaa na Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam zimeendelea kuhakiki pikipiki hizo ikiwa ni pamoja na kuwapangia maeneo ya kupaki.

‘’Kupitia usajili wa TRA na Serikali za Mitaa na Halmashauri za Jiji  zimeendelea kuhakiki pikipiki hizo    na kuanzisha utaratibu  wa kusajili katika maeneo ya maegesho   kupata kumbukumbu za miliki, dereva na eneo lake maalum la kuegesha,’’alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles