31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaipongeza Kampuni ya GBP kwa uzalendo

Susan Uhinga, Tanga

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameipongeza Kampuni ya uingizaji mafuta nchini ya GBP, kwa kuwa kampuni ya kizalendo inayopaswa kuigwa na kampuni nyingine.

Waziri Nditiye ametoa kauli hiyo mkoani Tanga leo Ijumaa Novemba 23, wakati alipotembelea uwekezaji wa bohari ya kampuni hiyo pamoja na kukagua miundombinu ya reli katika eneo la Ruvu Mluaza.

Amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo ni wa kuigwa na kulindwa ambao wamekuwa wakitumia miundombinu ya reli kusafirisha shehena zao za mafuta.

“Nasema ni wazalendo kutokana na kwamba mbali na kutumia reli yetu kusafirisha sheheni zao wamekuwa wanatusaidia hata kukarabati miundombinu hiyo,” amesema.

Aidha, Waziri Nditiye ametoa agizo kwa Shirika la Reli nchini kufanya ukarabati maeneo korofi ya miundombinu hiyo ili kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa watumiaji wa reli hiyo.

Naye Meneja wa Kampuni ya GBP mkoani Tanga, Amour Ally ameishukuru serikali kwa kuweka sera rafiki kwa wawekezaji, pia ameomba kurekebishwa kwa maeneo korofi ya reli ili kurahisisha shughuli za usafirishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles