23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAIKANA TAASISI INAYODAI KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI

 

DODOMA

SERIKALI imekana kuitambua Taasisi ya Mfuko wa Elimu ya Juu (TSSF), inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema hayo bungeni mjini Dodoma leo, wakati akitoa ufafanuzi baada ya Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) kuomba mwongozo kuhusu uhalali wa taasisi hiyo inayojinasibu kutoa mikopo kwa wanafunzi.

Amesema si wizara yake wala serikali inayoitambua taasisi hiyo ambayo imekuwa ikitoa matangazo kuwa inatoa mikopo.

“Nieleze kwa masikitiko kwamba nimepewa gazeti sasa hivi ambalo linaonyesha tangazo kwamba hii taasisi inawatangazia wanafunzi na inawatoza Sh 30,000 na wanasema watakuwa na mkutano ambao mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako.

“Siitambui taasisi hiyo, sitakuwa mgeni rasmi na wala hawajanikaribisha tarehe ya huo mkutano… kwa hiyo nitumie fursa hii kutoa tahadhari kwa Watanzania kwamba wawe makini kwa sababu unapoona mtu anatumia jina lako namna hii ni hatari.

“Kama serikali niseme tumelipokea na tutalifanyia kazi ili kujua uhalali wake, lakini kwa kipindi hiki nitoe tahadhari kwa watakaoamua kutoa hizo Sh 30,000 wafanye lakini wajue kwamba serikali hailitambui jambo hili,” amesema Profesa Ndalichako.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles