26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaanza kufufua shirika la uvuvi

Derick Milton, Simiyu

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeanza harati za kufufua shirika la Uvuvi nchini (TAFICO) ambalo kwa muda mrefu limekuwa halifanyi kazi na kusababisha serikali kushindwa kunufaika na rasilimali za uvuvi katika ukanda wa bahari kuu ya hindi.

Hayo yamebaishwa na Kaimu Meneja Mkuu wa shirika hilo, Ester Mulyila wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa kwenye Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Amesema kuwa shirika hilo kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu, imesababisha Watanzania kutonufaika na rasilimali uvuvi katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu tangu nchi ipate uhuru.

“Katika kufufua shirika hilo tumeanza na miradi mikuu mitatu, ambapo mmoja kati ya hiyo ni ununuzi wa meli mbili kubwa za uvuvi ambazo zitatumika kuvua samaki katika ukanda huo wa bahari kuu.

“Tutakuwa na meli kubwa mbili za uvuvi za kitaifa (National Fishing Fleet) ambazo zitafanya uvuvi katika ukanda huo wa bahari kuu pamoja na maji ya kitaifa ili kuiwezesha serikali kuongeza mapato yatokanayo na uvuvi, amesema.

Amesema miradi mingi ni ya uzalishaji wa vifaranga vya samaki pamoja na mradi wa kuchakata samaki ambapo wanategemea kuanzisha viwanda vya kuchakata huku shirika hilo likitegemea kupewa kiasi cha Sh bilioni 45 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles