33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ya Wilaya ya Mufindi kutumia azimio la dunia kushinda tuzo za mazingira

 Francis Godwin, Iringa

Serikali wilayani  Mufindi  mkoani Iringa imesema azimio la dunia la mabadiliko ya tabianchi lililotolewa katika kongamano la  wanafunzi  lililofanyika nchini Finland  watalitumia kama ya kitendea kazi  kwao  kuona  wilaya  hiyo inashinda  tuzo  mbali mbali  za uhifadhi wa mazingira .

Akizungumza leo Juni 19,   wakati akikabidhiwa azimio  hilo  kutoka kwa  Wanafunzi  Stephen Sanga na Mariam Wambura  wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga , Katibu  Tawala wa Wilaya hiyo,  Servi  Ndumbalo amesema atalikabidhi kwa  Ofisa Mazingira  wa  wilaya ili kulisoma  zaidi kabla ya  kulisambaza katika taasisi na shule  zote za wilaya   hiyo kwa utekelezaji .

 Ndumbalo ambaye  alimuwakilisha Mkuu  wa  Wilaya ya  Mufindi katika hafla  hiyo fupi ya kupokea azimio hilo la dunia  amesema   Wilaya   yake imepata  heshima  kubwa  ya  kuwakilisha nchi  kwenye  kongamano  hilo na hivyo wanatarajia  nafasi hiyo  kubwa waliyoipata  wanafunzi  fursa kwa  wilaya na Mkoa wa Iringa katika  utunzaji na uhifadhi wa mazingira .

Amesema  kwa  kupitia azimio   hilo  ambalo  limegawanyika katika  sehemu kuu tatu  wao kama  wilaya  watahakikisha  wanatekeleza  sehemu ya azimio  hilo ambayo imeigusa  serikali  ili kuona  shule  zote  zinafanikisha utekelezaji wa azimio  hilo kwa  wakati .

“Tunataka  wilaya ya  Mufindi  kuwa  mfano kwa  wilaya  nyingine nchini katika suala la  utuzaji wa mazingira  na kwa  kupitia azimio  hili  tutahakikisha  tutakwenda  hatua kwa  hatua  kuona  tunakidhi  vigezo vyote  vya ubora katika  utunzaji na uhifadhi wa mazingira  na ikiwezekana kushinda tuzo  mbali bali za mazingira  za  ndani na nje ya nchi ,”  amesema  Ndumbalo.

Amesema  maazimio  ya kongamano  hilo la wanafunzi  duniani lililomalizaka nchini Finland  watahakikisha  wanalitungia  kanuni  ili  kuweza  kulitekeleza kwa ufanisi na  kila mmoja atapewa  majukumu ya  kufanya  ili kufanikisha utekelezaji wa  maazimio  hayo .

Kwa  upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Mufindi, Netho Ndilito  akishukuru kwa  uwakilishi mzuri wa shule  hiyo ya Southern Highlands Mafinga katika  kongamano hilo  amesema   heshima ambayo  wanafunzi hao  wamerejea nayo ni heshima kwa  shule   hiyo na uongozi wake chini ya Mkurugenzi Mary Mungai na Kitova Mungai   na kwao serikali  watakuwa  bega kwa bega kuona shule  nyingine zinapewa elimu  ya mazingira .

Ndilito  alisema   kazi  hiyo   iliyofanywa na  shule hiyo  ni   kubwa na ndio lengo la serikali  kuona mazingira  yanaendelea  kutunzwa na miti inapandwa kwa  wingi ili  kuwezesha mradi mkubwa wa umeme  unaojengwa   kuendelea  kuwa  endelevu lakini dunia inaendelea  kuwa salama  bila  kukabiliwa na mabadiliko tabianchi .

Amesema   Halmashauri  yake  itahakikisha  inatoa ardhi ya  wazi  kwa  shule  hiyo ya na  shule  nyingine  za  wilaya    hiyo  ili  kupanda miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira na watawatumia wanafunzi hao wawili katika semina mbalimbali   kama mabalozi  wa  mazingira   na kuwaelimisha   wenzao juu ya mazingira .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles