30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, TPSF kukabili changamoto za uwekezaji

Mwandishi Wetu -Dodoma

SERIKALI na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), wameandaa mfumo wa kieletroniki wa kuwasilisha taarifa, ikiwamo malalamiko, maoni na kupata mrejesho ili kuinua daraja wa uwekezaji nchini na kuzidi kuboresha mazingira ya kufanya biashara ambao utaanza kutumika mwaka 2020/2021.

Akitangaza ubunifu huo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2020/2021, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisifu  mfumo huo na kusema kwamba utapunguza urasimu na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wawekezaji na kulieleza Bunge kwamba juhudi ya Watanzania kujiletea maendeleo ya kisasa inazaa matunda.

“Mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara vimeendelea kuimarika, na ushahidi huu inathibitishwa na taarifa ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia juu  ya Wepesi wa kufanya Biashara ya mwaka 2020.  Tanzania imepanda kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 144 hadi nafasi ya 141,’’ alisema Majaliwa 

Licha ya hali hiyo aliliambia Bunge kwamba mfumo huo wa kieletroki utaoneza  ufanisi zaidi katika ukuzaji uwekezaji na ufanyaji biashara nchini.

Aliahidi kwamba  serikali ikishirikiana na TPSF itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara  ili kupata nafasi za juu ya dunia  katika eneo hili. biashara.

Waziri Mkuu amezitaka taaasisi zote za serikali kuweka mazingira mazuri na rafiki kwa uwekezaji, kuimarisha uratibu wa ukaribu na kufungua fursa zaidi za uwekezaji na ufanyaji biashara.

 â€œSerikali itaendelea kuhamasisha mikoa yote nchini kuandaa makongamano ya uwekezaji  na kuzindua miongozo ya uwekezaji ya mikoa inayobainisha fursa za uwekezaji ili kufikia nafasi ya juu ya utendaji  ifikapo mwaka 2025,’’ alisema 

Waziri Mkuu  alisema kuwa serikali itahakikisha maeneo ya uwekezaji yanatengwa na kuendelezwa kwa kuwekewa miundombinu ya msingi .

“Juhudi kubwa imefanywa na serikali za mikoa kwa kuzindua miongozo ya fursa za kiuwekezaji ambapo jumla ya hekta 854,821 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo halmashauri zote nchini,’’ alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles