31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI, TANZANITE ONE MAMBO SAFI

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Tanzanite One, imekubali kuilipa serikali fidia na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwapo awali.

Fidia hiyo inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo, na haitahusisha kodi kwani italazimika kulipa kodi inazodaiwa na Serikali na tozo nyingine zote zinazodaiwa na Serikali kama kawaida.

Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam leo Mei 16, na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma.

Juni, mwaka jana wakati Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati ya madini iliyoongozwa na Abdulkarim Mruma, aliagiza kukamatwa wakurugenzi wa Tanzanite One, Hussein Gonga na Faisal Juma kutokana na kuguswa kwenye ripoti hiyo lakini siku chache baadaye akiwa ziarani mkoani Manyara.

Rais aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwaachia huru wawekezaji hao katika migodi ya Tanzanite One waliokamatwa kwa ajili ya kusaidia kutoa taarifa nyeti na kukaa na kamati ya kujadili madini kurekebisha mkataba utakaokuwa na faida kwa serikali na si wa unyonyaji.

Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekitiwa wa kamati hiyo, Profesa Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa fidia kutokana na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioleta hasara kwa Serikali.

“Pia Serikali imekubaliana na Kampuniya Tanzanite One kuwa itafuata masharti yote ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaeleza kuwa ni Watanzania tu ndiyo wanaoruhusiwa kuchimba madini ya vito na pale ambapo Watanzania hawana uwezo huo ndipo wanapoweza kuingia ubia na wageni,” amesema Profesa Kabudi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuniya Tanzanite One, Faisal Juma wamejadiliana na serikali na kufikia muafaka na itahakikisha inafuata taratibu kwa lengo la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles