27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUTOA AJIRA MPYA 49,000

Na FRED AZZAH-DODOMA


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amesema mwaka ujao wa fedha Serikali itaajiri watumishi 49,356 kwenye sekta mbalimbali.

Mkuchika alisema hayo bungeni jana wakati akihitimisha hotuba ya Makadrio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Alisema, kati ya   hizo,  ajira 16,000 zitakwenda kwa walimu wa shule za msingi na sekondari huku afya ikichukua ajira 15,000 na zilizobaki zitakwenda upande wa kilimo, uvuvi mifugo, vyombo vya ulinzi, magereza, uhamiaji, watendaji na wahadhiri wa vyuo.

Mkuchika alisema  kati ya ajira 52,000 zilizotangazwa mwaka jana, mpaka Machi mwaka huu Serikali imekwisha kuajiri watumishi zaidi ya 18,000 kuziba maeneo yenye upungufu.

Alisema katika bajeti hiyo inayoishia Juni 30 mwaka huu, watajiriwa watumishi wengi kutoka  idara ya elimu, afya na Serikali za mitaa  kutimiza idadi ya 52,000.

Waziri alisema watumishi hao tayari walikwisha kupitishwa katika bajeti iliyopita.

Kuhusu kupandisha vyeo watumishi, alisema kwa mwaka ujao watumishi 162,221 watapandishwa vyeo katika kada mbalimbali.

Katika orodha hiyo, watumishi 2,044 watapandishwa vyeo kuziba mapengo ya vyeo katika ngazi ya madaraka.

Alisema uteuzi huo utapunguza nafasi nyingi ambazo kwa sasa zimekaimiwa.

Kuhusu nyongeza ya mishahara, waziri  alisema Serikali inakusudia kutoa nyongeza ya mwaka kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

Akizungumzia  utawala bora, Mkuchika alisema wabunge wamelalamikia watu kutekwa,  kupigwa na upendeleo mwingi.

Waziri alisema Serikali haiungi mkono mambo hayo na ndiyo maana huchukua hatua mara moja   vitendo hivyo vinapojitokeza.

“Jeshi lenye dhamana na usalama wa raia ni polisi, si idara ya usalama wa taifa. Natoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo,” alisema.

Mkuchika alisema Serikali haina ushahidi wa  viongozi wa dini kupata misukosuko kama baadhi ya wabunge walivyodai.

“Ukitaka kumshauri mzee wako huitishi mkutano wa hadhara, hakuna njia ya kumfikia baba yako kimyakimya,”alisema.

Kuhusu Diwani wa Kakonko (CCM) aliyepotea, alisema serikali haipuuzi kupotea kwa watu nchini na   uchunguzi unaendelea wa tukio hilo baada ya kuripotiwa kwa Jeshi la Polisi.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, alisema mpaka kufikia Februari, fedha za maendeleo zilizokuwa zimetolewa ni asilimia 50 ya bajeti iliyotengwa.

Kuhusu bajeti la lishe, alisema kwa mwaka wa fedha ujao imeongezwa na kufikia Sh bilioni 15 kutoka Sh bilioni 11 mwaka uliopita.

Akizungumzia fedha za maendeleo, alisema hadi Februari mwaka huu zilikuwa zimetolewa Sh bilioni 914.39 (asilimia 50) ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Kuhusu elimu bure, alisema kuanzia Desemba mwaka 2015  Serikali ilikuwa ikitoa bajeti ya elimu bila malipo ya Sh 23bilioni.

Hata hivyo, alisema mwaka jana walikwama na   hata wabunge wengine walilamikia kuwa kiasi hicho cha fedha hakitoshi.

“Tulimuomba Rais akasema tusubiri bajeti hii na bahati nzuri sasa tumepata addition (nyongeza) ya fedha karibu Sh bilioni 3.6   ambazo zinaongezeka katika bajeti,”alisema.

Kuhusu mishahara kumeza bajeti, Jafo alisema matumizi makubwa ya fedha yanakwenda katika matumizi mengine.

Alisema  bajeti ya matumizi ya kawaida kwa wizara hiyo mwaka jana ilikuwa Sh trilioni 7, kati yake zaidi yake Sh trilioni  4  zikiwa ni mishahara.

“Bajeti nzima ya mishahara katika wizara hii inachukua asilimia 56 ya mishahara ya nchi nzima,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles