30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kujenga kituo cha pamoja cha madini Mirerani

Bethsheba Wambura

Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa wa kituo cha pamoja cha biashara ya madini ‘One Stop Centre’ kitachojengwa Mirerani mkoani Manyara.

Kituo hicho kitakachogharimu Sh bilioni 1.148 ambapo wafanyabiashara wa madini yote wataweza kufanya biashara zao kwa urahisi.

Ujenzi wa kituo hicho umetokana na agizo alilolitoa Rais Dk. John Magufuli, Januari 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa wachimbaji wadogo na wadau wa madini la kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara ya madini ya Tanzanite na kuimarisha usalama kwa kuweka mifumo ya kidigitali ya ulinzi kuzunguka ukuta.

Akizungumza leo Jumapili Februari 16, wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho na uzinduzi wa jengo la madalali na uthaminishaji wa madini ‘Brokers House’ ambalo litakuwepo ndani ya ukuta wa Mirerani, Waziri wa Madini, Dotto Biteko, amesema litawasaidia wafanyabiashara wadogo na wenye madini kufanya biashara sehemu salama na yenye uwazi.

Waziri huyo pamoja na kuzindua majengo hayo pia amekabidhi barua kwa mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kuweka mifumo ya ulinzi ya kieletroniki kuzunguka ukuta wa Mirerani kama Rais Magufuli alivyoelekeza, ambayo itawezesha kuona kila kinachoendelea Mirerani hata kama mtu yupo mbali.

“Jengo hili la Brokers House lililogharimu Sh milioni 85 limejengwa baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wafanya biashara wa madini ya Tanzanite kuwa hakuna sehemu ya kufanyia tathmini.

“Lakini pamoja na kuzindua jengo hilo nitaweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi ambao tayari umeshaanza wa jengo la biashara ya pamoja ambapo huduma zote za kibiashara na kiserikali zitapatikana na niwakikishie tu kuwa ujenzi huu unakidhi matakwa yote ya kibiashara na kiusalama kwa mnunuaji na muuzaji,” amesema.

Aidha, Waziri huyo amemtaka mkandarasi kumaliza ujenzi kwa wakati na kuweka mifumo yote inayotakiwa ili kuleta tija iliyokusudiwa, lakini pia ametoa rai kwa wafanyabiashara wa madini kufanya uuzaji na ununuaji wa madini katika eneo maalumu linalojengwa mahsusi kwa biashara hizo ili kukwepa usumbufu na mfanyabiashara yeyote atakayekamatwa akitorosha madini atachukuliwa hatua kali ikiwamo kutokuruhusiwa kuingia katika machimbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles