Imechapishwa: Fri, Sep 29th, 2017

SERIKALI KUISAPOTI TFF AFCON U-17

WINFRIDA MTOI NA TIMA SIKILO

SERIKALI imesema itakuwa bega kwa bega na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katika kuhakikisha maandalizi kuelekea michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanakwenda vizuri.

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa AFCON kwa vijana iliyopangwa kufanyika mwa 2019 na tayari kamati ya maandalizi ya ufundi imeundwa.

Kamati hiyo inaongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, Yusuf Singo, katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, mkurugenzi wa ufundi TFF, Salum Madadi, Henry Tandau na Kasongo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Waziri wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, alisema uandaaji wa fainali hizo haujaja ghafla  hivyo ni lazima maandalizi yafanyike kamainavyotakiwa.

Mwakyembe alisema hayo wakati alipokutana na kamatihiyo kwa mara ya kwanza na kusema wakishindwa watakuwa hawana cha kuwaambia Watanzania  kwa sababu ni suala walilolijua muda mrefu.

“Tuliomba wenyewe mwaka 2013 kuandaa mashindano haya na 2015, tukajibiwa na kupewa nafasi hiyo, ninaamini tutafanya vizuri. Kazi ya maandalizi inakwenda vizuri. Wanaofanyia uwanja wa Taifa ukarabati wameahidi baada ya miezi mitatu watatukabidhi,” alisema Mwakyembe.

Alieleza kuwa  wiraza inatarajia kupata  fedha katika bajeti inayokuja kwa ajili ya michuano hiyo huku wakiendelea kushirikiana na wadau wengine kama ilivyotokea kwenye ukarabati wa uwanja.

Aidha Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Leodgar Tenga, alisema  atatumia nafasi yake katika kuhamasisha maandalizi kwa kuwa anajua mahitaji yanayotakiwa ni mengi.

Rais wa TFF, Wallace Karia alisema  maandalizi  yalinza muda mrefu kwa kuandaa timu ya vijana ambayo Novemba mwaka huu itarejea tena kambini.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

SERIKALI KUISAPOTI TFF AFCON U-17