27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUFUNGUA OFISI ZA TAKWIMU NCHI NZIMA

NA ASHA BANI -DODOMA

SERIKALI  ipo katika ukamilishaji wa kuanzisha ofisi za Takwimu katika halmashauri nchini kwa lengo la kusaidia kukusanya taarifa za elimu na kuzifanyia kazi ili kuleta ufanisi katika sekta ya elimu.

Pia imefanikiwa kusambaza vitabu milioni 14.51 sawa na asilimia 32.81 kati ya vitabu vilivyopangwa kusambazwa ambavyo ni milioni 44.24 vya elimu ya awali, darasa la kwanza hadi la tatu .

Lengo hadi kufikia Juni mwakani vitabu milioni 27.74  sawa na asilimia 62.72 viwe vimechapwa na kusambazwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na Mratibu Msaidizi wa Programu ya Ujifunzaji na Ufundishaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Isack Kitururu alisema programu hiyo iliyoanza mwaka 2014 na inarajiwa kumalizika Desemba 2018 kwa ufadhili wa Serikali ya Sweden wa Dola milioni 94.8.

Alisema mpang huo umejikita kwenye maeneo makuu matatu ambapo ni  kujenga uwezo wa kujifunza na kufundisha wanafunzi kati ya miaka 5 hadi 13 waweze kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), kuwajengea uwezo walimu, jamii na kamati za shule.

Alisema ili kuweza kufanikisha programu hiyo ni lazima kuwepo na jitihada za makusudi kuhakikisha kunakuwa na ofisi za takwimu ambazo zitafanikisha ukusanyaji wa data za elimu na utekelezaji wa  programu hiyo katika shule zote.

“Katika mpango wa KKK wizara ina imani tatizo la watoto kutokujua kusoma wala kuandika litakua historia kwani unaanza hatua ya awali na akifika la kwanza , la pili hadi la tatu anajua kusoma.

“Kuwapima watoto itasaidia kwa jamii kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani na walimu kufahamu mtoto mwenye matatizo ya usikivu au uoni hafifu kukaa mbele bada ya nyuma ya darasa,’’ alisema Kitururu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles