25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kufufua viwanda vilivyokufa Kilimanjaro

Safina Sarwatt – Hai

Serikali imeanza  utekelezaji wa kufufua  kiwanda cha kutengeneza vipuli  vya viwandani  na magari  cha Mashine tools kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, ambacho kilisimamisha uzalishaji kwa zaidi ya mika 30.

Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashunga amethibitisha jambo hilo leo Alhamisi Julai 4, wakati wa akizindua matengenezo ya tela za trekta mpya katika kiwanda hicho ambapo amezitaka taasisi zinazotengeneza  zana za viwandani kuzalisha bidhaa bora zitakazowasaidia wakulima wadogo ili kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa tayari serikali imeridhia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro la kufufua viwanda ambavyo vimekufa kwa muda mrefu na kwamba lazima mkakati huo uende sambamba na kubadilisha maisha ya wakulima wadogo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, amesema mpango wa kufufua kiwanda hicho kitakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi mkoani humo na kwamba kuna wawekezaji kutoka nje ambao wameonyesha nia ya kuja kuwekeza katika kiwanda hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles