23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUENDELEZA KILIMO KWA MFUMO WA SAGCOT

Serikali inaanza mkakati wa kuendeleza kilimo nchini kwa kutumia mfumo wa  Mpango wa Kuboresha Kilimo kwa Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) mwaka huu wa fedha 2017/18.

Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Yongolo Said amesema lengo ni kuhakikisha kilimo kinalisaidia taifa kufikia malengo ya uchumi wa viwanda, imefahamika.

Alikuwa akizungumza katika hafla ya  kazi  iliyowaleta pamoja maofisa wa Serikali kutoka wizara na idara mbalimbali zinazofanya kazi kwa karibu na SAGCOT mwishoni mwa wiki.

Alisema serikali imekamilisha utaratibu wote kuhakikisha mfumo wa SAGCOT unatumika kuendeleza kilimo nchini kote.

Hivi sasa  mfumo wa SAGCOT hutumika katika maeneo ya kusini mwa nchi ambako umeonyesha mafanikio makubwa katika kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikidhi katika maisha na kuwa cha  biashara.

SAGCOT ni mfumo wa kuendeleza kilimo unaozileta pamoja taasisi za umma, binafsi na wafadhili wa kimataifa ukiwa na lengo la kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo kwa pamoja.

“Kimsingi, mwaka huu wa fedha tunaanza kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2) ambako tumeiga mambo mengi kutokana na mafanikio ya SAGCOT.

“Kama serikali  tumetambua kuwa SAGCOT ndiyo mfumo bora wa kuendeleza kilimo nchini na ndiyo maana sasa tunaupeleka nchi nzima kwa kupitia ASDP 2,” alisema.

Said ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvivu alisema   pia alipata nafasi ya kujua mambo mengi yaliyofanywa kwa usimamizi wa SAGCOT katika eneo lote la mradi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha SAGCOT, Geoffrey Kirenga, alisema lengo la SAGCOT ni kutumia utaratibu wa biashara unaolenga kuwezesha uwekezaji katika kilimo unaofikia Dola za Marekani bilioni 3.5 ifikapo mwaka 2030.

Kati ya fedha hizo, Dola bilioni 2.1 zitawekezwa na sekta binafsi na zilizobaki zitawekezwa na serikali.

Hekta 38,477 zinalimwa kwa mfumo wa SAGCOT ambako wakulima hupata Dola za Marekani 50 milioni kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles