SERIKALI KUDHIBITI MFUMO WA KUTANGAZA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

0
466

|Mwandishi Wetu, Dar es SalaamSerikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha mfumo madhubuti wa kutoa matangazo yake na taasisi zake katika vyombo mbalimbali vya habari nchini utakaodhibiti maofisa wake kutotoa matangazo kiholela.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abasi, amesema hayo leo Ijumaa Agosti 24, wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa New Habari (2006) Ltd.

Amesema hatua hiyo inatokana na changamoto iliyogusa biashara ya matangazo serikalini na kuongeza kuwa amekuta barua nyingi za vyombo vya habari zikidai madeni yao yanayotokana na matangazo.

“Ni madeni ambayo serikali inadaiwa kwa kutangaza, ambayo kwa namna namna tofauti ya kufanya matangazo mlitangaza

“Vyombo vya habari karibu vyote, nafikiri hata wahariri kwenye moja ya tamko lao walilisema hilo lakini waliliweka kwenye namna ambayo asiyeelewa hawezi kuelewa, lakini tulioelewa tulielewa.

“Hii biashara ilikuwa holela holela, kwa hiyo nimekuta mafaili na barua, mimi sikuwepo yaani watu wanaingia makubaliano kienyeji tu wanatangaza, sasa shughuli imekuja kuanza, mnarudi huku kuhakikiwa bajeti ilikuwapo, haikuwepo,” amesema Dk. Abasi.

Pamoja na mambo mengine, amesema kama kuna kesi kubwa zinazochangia hali mbaya kwa vyombo vya habari ni hiyo hali kwamba watu waliingia mikataba ya kutangaza hayo matangazo ambapo yule ofisa anayeingia naye alikuwa anaiwahi hiyo asilimia 10 (commission) ya matangazo hayo.

“Wewe unaongea naye huyo ofisa haraka haraka  anakwambia mimi nakuletea matangazo yangu lakini utaniletea kamisheni yangu, kumbe kule ofisini hakuna bajeti hiyo iliyotengwa kwa mwaka huo kwenye ofisi yake kwa hiyo huku kashakuingiza mkenge.

“Kwa hiyo sehemu kubwa ya madai nayahakiki, naanzia huyo aliyekuruhusu utangaze, aidha yupo au hayupo, alikuwa na mamlaka gani ya kukuruhusu wewe utangaze.

“Lakini mimi nasema kama mwanataaluma, ni athari kwetu na naomba mturuhusu tubadilishe huu mfumo,” amesema Dk. Abbasi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here