Serikali yaagiza kuchunguzwa kwa afya za wachezaji

0
438

Ramadhan Hassan,Dodoma

Serikali imeziagiza  Klabu za michezo kuhakikisha wanawachunguza na kuwapima afya  wachezaji kabla ya kuwasajili na kabla ya mashindano mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo Mei 31, bungeni na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Juliana Shonza,wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nungwi,Haji Khamisi (CUF).

Katika swali lake,Khamisi amesema tatizo la wachezaji kuanguka na kufariki uwanjani limekuwa kubwa,Je Waziri yupo tayari kuviagiza Klabu kupima afya zao kwa ulazima.

Akijibu,Naibu Waziri Shonza amesema suala la kupima afya ni agizo ambalo pia lipo katika kanuni za TFF na FIFA hivyo alizitaka Klabu kuhakikisha wanawapima wachezaji kabla ya mashindano na kabla ya kuwasajili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here