31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

‘SERIKALI IMALIZE TATIZO LA VYOO SHULENI’

shule-zetu

NA CLARA MATIMO- MWANZA


 

SERIKALI imeshauriwa  kutatua tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi wa shule za msingi nchini, ili kuwaepusha kupata magonjwa ya mlipuko.

Ushauri huo ulitolewa  jana na Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji  Ubongo na Uti wa Mgongo  wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), Dk. Emmanuel Kanumba, alipozungumza na MTANZANIA  kuhusu athari ambazo wanafunzi wanaweza kuzipata kutokana na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Dk. Kanumba, alisema   endapo wanafunzi watakabiliwa na upungufu wa  matundu ya vyoo wanaweza kujikuta wakiambukizana mradhi mbalimbali kutokan ana kujisaidia ovyo  nje ya majengo ya shule.

Hali hiyo  husababisha kuibuka kwa magonjwa yaenezwayo kwa njia ya hewa na  kushikana mikono  kwa sababu shule nyingi hazina maji.

“Magonjwa ya mlipuko huenea kwa kasi na madhara yake ni makubwa kwa sababu husababisha vifo vingi endapo wagonjwa hawatapata matibabu sahihi kwa wakati.

“Naishauri Serikali ilipe suala la matundu ya vyooo katika shule za msingi  kipaumbele kwa sababu wanafunzi wanaosoma shule hizo bado ni watoto.

“watoto wa shule za msingi siku hizo ni wadogo na hawana uwezo wa kujikinga na kujilinda ni mwanafunzi wa darasa la kwanza au la pili akihitaji kujisaidia akienda chooni akamkuta mwenzake hawezi kuvumilia atajisaidia nje ya tundu la choo, kuzuia ni bora kuliko kutibu,”alisema.

Aliiomba  Serikali  kulipa kipaumbele suala la matundu ya vyoo hasa kwa shule za msingi ili kuepuka kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko kama kipundupindu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles