27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, familia wamaliza mzozo mazishi ya Mugabe

HARARE, ZIMBABWE

SERIKALI ya Zimbabwe na familia ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe wamefikia mwafaka wa kiongozi huyo kuzikwa katika makaburi ya Mashujaa wa Taifa hilo mjini Harare.

Msemaji wa familia na mpwa wa  Mugabe, Leo amesema tarehe bado haijajulikana.

Kabla ya kuzikwa kutakuwa na shughuli ya wazi ya umma katika makaburi ya kitaifa mjini  Harare siku ya Jumapili.

Leo ambaye alizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC alisema baada ya shughuli hiyo itafuatia nyingine ya kimila ambayo itafanyika kijijini  Kutama ambako ni nyumbani kwa Mugabe na itaendeshwa na viongozi wa ukoo na kimila wakiwamo machifu.

Jana mwili wake ulikuwa katika uwanja wa Rufaro kwa ajili ya kuwapa nafasi wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Kabla ya taarifa hizo mpya Rais  wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa alifika nyumbani kwa Mugabe na kuzungumza na mkewe, Grace akisema hakuna uamuzi utakaofanywa kuhusu mazishi ya rais  huyo wa zamani kinyume na matakwa ya familia yake.

Zaidi Rais Mnangangwa alimuhakikishia mke wa marehemu Mugabe, Grace kwamba anayo sapoti ya serikali.

Kauli hiyo ya Rais Mnangagwa ilikuja baada ya mzozo juu ya mahali ambako atazikwa, Mugabe ukioneakana dhahiri juzi baada ya familia yake kusema imeshutushwa kwa kutopewa nafasi ya kushauriana na Serikali juu ya mipango ya mazishi ya kiongozi huyo.

Kauli hiyo ilitolewa baada ya mwili wake kuwasili nchini Zimbabwe ukitokea Singapore alikokuwa akitibiwa kabla ya mauti kumfika Ijumaa iliyopita.

Kutokana na hilo Familia yake ilitoa taarifa ambayo mbali na kuweka msimamo wa mahali atakakopumzishwa pia ilibadili siku ambayo Mugabe atazikwa.

Familia yake ilisema mwili wake utalazwa na kuonekana mara ya mwisho nyumbani kwake katika kijiji cha Kutama Jumapili usiku.

Kabla ya uamuzi wa sasa ilitaka azikwe katika mazishi ya faragha kati ya Jumatatu au Jumanne.

Katika taarifa hiyo ya familia,  ileleza kuwa kuwa ratiba ya mazishi ya Mugabe iliyopangwa na Serikali ilikuwa inakwenda kinyume na wosia wake wa kutaka mwili wake uhifadhiwe.

Taarifa hiyo ilitaja mojawapo ya maombi ya marehemu Mugabe ilikuwa ni kutaka mkewe, Grace Mugabe, asiondoke karibu na jeneza lake wakati wa mazishi mpaka atakapozikwa.

Familia ya Mugabe inasemekana kuwa na uchungu kwa namna Mugabe alivyotimuliwa na aliyekuwa mshirika wake ambaye kwa sasa ni Rais wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa miaka miwili iliyopita.

Akizungumza nyumbani kwa Mugabe ambako viongozi na wananchi mbalimbali walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuomboleza kifo chake, Rais Mnangagwa alisema;

“Amai (mke wa rais wa zamani Grace Mugabe), una sapoti yote ya Serikali chini yangu, wale watakaoongeza watafanya hivyo, lakini kama Serikali  

lakini kama Serikali hakuna kitu ambacho tutafanya tofauti na matakwa yako,” alisema.

“Je! Atazikwa wapi na jinsi gani, hatujatoa taarifa bado  hadi tukutane na Amai ili tushirikishane pamoja. Wakati mama yangu alipofariki, Rais wa zamani (Mugabe) alikuja nyumbani kwangu na alikaa kwa muda kabisa.

“Tutajaribu kufanya maandalizi yote. Nataka familia itambue kuwa serikali inayoongozwa na Zanu-PF haitasahau kwamba tuna kiongozi wetu, ni jambo ambalo tunalifanya kama utamaduni.

“Wacha tuwe na roho ya umoja na upendo. Ukizingatia Zanu-PF ipo madarakani na ninaongoza,  hakuna mtu anayeweza kubadili hilo kwamba; atabaki kuwa nembo yetu na kamanda, hatuwezi kubadilisha hili.” Alikaririwa  Rais Mnangagwa na gazeti la serikali la nchini humo la The Herald.

Rais Mnangagwa alisema tangu awe Mkuu wa Nchi na Serikali, amejitahidi kutimiza mahitaji yote ambayo mke huyo wa Rais zamani aliyahitaji.

“Kuanzia siku ambayo nilichukua madarakani, hakukuwa na ombi ambalo nililikataa,kama msaada hata safari ya matibabu  ya kiongozi wetu Singapore,”  alisema.

Alipotembelea nyumbani hapo Rais  Mnangagwa alitoa heshima za mwisho kwa Mugabe ambaye amefanya naye kazi kwa muda mrefu.

“Nilifanya naye kazi kwa zaidi ya miaka 54, kutoka mwaka 1962,” alisema.

 “Mwaka 1963 nilipofungwa alinisaidia kufanya taratibu za kunitoa jela. Hatukuwahi kuwa na tatizo naye, isipokuwa lile lililotokea ambalo wote mnalijua, lakini niliporudi nyumbani nilisema tuyaache ya kale yawe ya kale, hiyo ndiyo roho niliyonayo.”

Wakati huo huo, Rais Mnangagwa alikosoa baadhi ya vyombo vya habari kwa kutia chumvi kuhusu idadi ya viongozi kutoka mataifa mengine ambao wamethibitisha kushiriki  shughuli ya mazishi ya Mugabe leo katika uwanja wa taifa wa michezo.

Juzi gazeti la nchini humo la Daily News liliorodhesha orodha ya viongozi 49 kutoka katika mataifa mbalimbali duniani ambao ilidai kuwa wamethibitisha kushiriki shughuli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles