24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serengeti Boys kujipima kwa Azam leo

serengeti boys
serengeti boys

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, leo inatarajia kucheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Azam U-20 katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Dar es Salaam jana kuwa, mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boys likiongozwa na kocha, Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.

Alisema Serengeti Boys itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini ‘Amajimbos’ Julai 18, mwaka huu katika uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.

Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles