SERENA ATOZWA FAINI

0
614

Marekani


Mchezaji wa Tenesi nchini Marekani, Serena Williams, ametozwa faini dhidi ya kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya kwenye michuano ya wazi ya tenesi ya Marekani.

Williams, 36, ametozwa faini ya dola 17,000 sawa na shilingi milioni 38.7 kwa kukiuka kanuni za mchezo wa Tenesi ikiwa ni pamoja na kumuita mwamuzi Umpire Carlos Ramos, muongo na mwizi.

Hata hivyo mchezaji huyo amejishindia dola milioni 1.85 sawa na shilingi bilioni 4.2 kwa kufuzu kuingia fainali ya mashindano hayo.

Mwamuzi Carlos Ramos, alimuadhibu Williams, baada ya kumuona mkufunzi wake Patrick Mouratoglou, akionyesha ishara ya mkono. Baadaye mkufunzi huyo raia wa Ufaransa alikiri kuwa alijaribu kumuelekeza mchezaji wake.

Mkuu wa shirikisho la mchezo wa Tenisi nchini Marekani (USTA) Katrina Adams, amesema wachezaji wakiume wamekuwa wakiwakaripia waamuzi wakati wa kubadilishana upande wa kuchezea na hatuoni chochote kikitokea.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here