24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SELENA, THE WEEKND ‘WABWAGANA’

NEW YORK, MAREKANI

KWA mujibu wa mtandao wa TMZ, mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Selena Gomez na mpenzi wake nyota wa muziki Abel Tesfaye ‘The Weeknd’, wanadaiwa kuachana baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miezi 10.

Kuachana kwa wawili hao kumekuja mara baada ya wiki iliyopita Selena kuonekana akiwa na mpenzi wake wa zamani, Justin Bieber.

Taarifa za Selena na Bieber kuwa pamoja zilianzia kanisani walipokuwa wanasali, lakini wamekwenda mbali zaidi na kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja na kuvaa nguo ambazo zinafanana, lakini hawajaweka wazi kama wamerudiana.

Tangu Bieber na Selena waonekane pamoja, mrembo huyo amegoma kuzungumzia suala la uhusiano wake na The Weeknd, lakini The Weeknd wiki iliyopita alisema hakuna chochote kinachoendelea kati ya Bieber na Selena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles