25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SEKTA ZA AFYA ZAASWA KUFUATILIA MIKATABA YAKE

 

Halmashauri za Wilaya za Kilwa, Nachingwea na Lindi zimetakiwa kufuatilia kwa karibu mikataba ya utoaji huduma za afya baina ya sekta za umma na watoa huduma za afya binafsi kwa kushirikiana na timu za Afya za Halmashauri na Mkoa ili kuona yanyofanyika katika mikataba hiyo.

Mratibu wa ushirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mariam Ongara amesema hayo wakati wa utiaji saini mkataba wa utoaji wa huduma za Afya baina ya sekta hizo mbili.

“Hili ni jambo la msingi sana kwa sababu kusaini mkataba ni jambo moja na kufuatilia utekelezaji wa mkataba huo ni jambo jingine, kwa hiyo ufuatiliaji wa mkataba ni jambo muhimu sana maana hiyo ndiyo changamoto inayotukabili katika utekelezaji wa mikataba kama hiyo,” amesema Dk. Ongara.

Amesema ili waendelee kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi wetu ni vyema mikataba hii ikawa endelevu ingawa ipo changamoto katika ufuatiliaji wa mikataba hiyo na ndiyo maana amezitaka halmashauri zilizohusika kufuatilia kwa karibu.

Ongara pia amesema ushirikiano baina ya sekta za umma na binafs ni suala mtambuka ambalo ni kipaumbele cha Serikali kwa Wizara ya Afya kwa  mkakati uliopo katika wizara hiyo wa ubia na ushirikiano wa sekta binafsi na sekta za umma wa mwaka 2015 mpaka mwaka 2020

“kutokana na hali hiyo serikali tunatekeleza mikakati yote ambayo ipo kwenye mkakati huo wa ubia na ushirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi” amesema Dk. Ongara.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles