29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SAYARI YA MARS ILIKUWA NA UWEZO WA KUHIFADHI VIUMBE HAI

Na JUSTIN DAMIAN



MIAKA kadhaa iliyopita, sayari ya Mars ilikuwa ni sehemu nzuri ambayo viumbe hai wangeweza kuishi kutokana na uwepo wa maji ya kutosha pamoja na udongo wenye rutuba, wanasayansi wanasema.

Tumegundua mazingira ambayo yangeweza kufaa kwa maisha ya viumbe hai ikiwemo uwepo wa maji ambayo kama yangekuwepo duniani tungeweza kuyatumia kwa ajili ya kunywa na shughuli nyingine,” anasema John Grotzinger ambaye ni Profesa katika taasisi ya Teknalojia ya California nchini Marekani.

Profesa Grotzinger pia ameshiriki katika utafiti kuhusu Mars kupitia Kituo cha Anga cha Marekani (NASA).
Kupitia roboti aliyetumwa kufanya utafiti kwa kupasua mwamba na kuteta taarifa zake duniani, wanasayansi wanasema uwepo wa matope katikati ya miamba ni ushahidi tosha kuwa miaka iliyopita sayari hiyo ilikuwa na maji ya kutosha.

Pamoja na maji, wanasayansi waligundua madini kama, sulfur, nitrogen, hydrogen, oxygen, phosphorus na carbon kwenye miamba ambayo ni muhimu kwa maisha.
Profesa Grotzinger anasema madini hayo ni kama betri na ni muhimu kwa maisha kwa kuwa ni chanzo cha nishati kwa mwili.

Ugunduzi mwingine muhimu ni pamoja na udongo wa mfinyanzi ambao mara nyingi hupatikana sehemu zenye maji
“Kitu muhimu ambacho tumeweza kujifunza ni kuwa, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita baadhi ya viumbe wadogo wadogo wangeweza kupata nguvu kwa kula kupitia miaka ambayo ilikuwa na madini muhimu kwa maisha,” anasema Grotzinger.

Hata hivyo wanasayansi wanasema, takribani miaka bilioni tatu iliyopita, hali katika sayari ya Mars ilibadilika. Mabadiliko hayo yalihusisha kupoa kwa hali ya hewa pamoja kusimama kwa ulipukaji wa volacano. Maji yaliganda au kutoweka kwa njia ya mvuke na kuifanya sayari hiyo kuwa kavu na yenye baridi.

Leo hii uso wa sayari hiyo ni baridi na mkavu huku ukiwa na mionzi inayotokea angani. Lakini wanasayansi wanaamini kuwa miaka bilioni tatu iliyopita ilikuwa ni sehemu nzuri kwa maisha kwa kuwa hali ya hewa ilikuwa ya baridi ya wastani pamoja na maji yaliyokuwa yakitiririka.

Ujumbe wa NASA ulioenda Mars haukuwa na chombo chenye uwezo wa kutambua kama kuna kiumbe aliwahi kuishi kwenye sayari hiyo, lakini iliweza kutambua baadhi ya madini ambayo kimsingi ni muhimu kwa maisha.
“Ninayo picha sasa ya kitu kama ziwa la maji baridi pamoja na hali ya hewa ya wastani kwa ajili ya maisha,” anasema John Grunsfeld, mmoja kati ya timu inayofanya utafiti juu ya Mars kutoka NASA.

Sayari ya Mars ni ya nne kwenye mfumo wa jua na ni ya pili kwa udogo. Jina la Mras lilitokana na mungu wa vita wa dola ya Warumi ya zamani. Sayari hii wakati mwingine hujulikana kama Sayari Nyekundu kutokana na kuwa na muonekano wenye rangi nyekundu.

Pamoja na utafiti wa miaka mingi, hakuna binadamu amefanikiwa kufika katika sayari hii kutokana na sabau mbalimbali ikiwamo hali ya hewa ya baridi sana pamoja na hewa ya carbon dioxide
Kama binadamu akifanikiwa kufika kwenye sayari hii, atajikuta akiwa na uzito mdogo kuliko uzito wake halisi kutokana na nguvu ya gravity. Endapo ana kilo 45 akifika Mars atajikuta akiwa na kilo 17.

Kama ilivyo kwa dunia, Mars ina majira aina nne lakini kwa saizi ni ndogo ukilinganisha na dunia.
Sayari hii pia ina mlima mkubwa zaidi unaoshikilia nafasi ya pili katika mfumo wa jua unaojulikana kama Olympus Mons ambao ni mrefu kuliko mlima wowote uliopo duniani. Mlima huu unaaminika kuwa ulikuwa na volcano lakini kutokana na mabadiliko ndai ya sayari hiyo, volcano hiyo imegeuka kuwa mfu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles