Imechapishwa: Fri, Jan 12th, 2018

SAUTI ZA BUSARA KURINDIMA ZANZIBAR FEBRUARI 8

Na MWANDISHI WETU- ZANZIBAR

SHEREHE za uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la muziki wa Afrika Mashariki, Sauti za Busara, zinatarajiwa kufanyika Februari 8 kwenye mji wa Stone Town, visiwani Zanzibar.

Tamasha hilo la 15 linalojumuisha wasanii mbalimbali wakiwemo wakimataifa na wandani, pia wapo watakaoonyesha umahiri wao kupitia makundi ya ngoma za asili hadi mwisho wa tamasha hilo Februari 11.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud maarufu Dj Yusuf, alisema zaidi ya wasanii 460 akiwemo Saida

Karoli na Grace Matata wa Tanzania watashiriki huku akitaja baadhi ya nchi zitakazoshiriki kuwa ni Algeria,

Burundi, DRC, Misri, Kenya, Malawi, Morocco, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Uganda na Zimbabwe.

Dj Yusufu alitaja baadhi ya makundi mengine kuwa ni Kasai Allstars (DRC), ZakesBantwini (Afrika Kusini), Somi (Uganda / USA), Msafiri Zawose (Tanzania), Ribab Fusion (Morocco), Kidum & Bodaboda Band (Burundi / Kenya) na Mlimani Park Orchestra kutoka (Tanzania).

Dj Yusuf aliongeza kwamba katika tamasha hilo kutasaidia kukuza uchumi wa Zanzibar kupitia sekta yake ya utalii, lakini pia itasaidia kuongeza ajira kwa vijana kupitia mambo mbalimbali ikiwemo fursa za kibiashara.

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

SAUTI ZA BUSARA KURINDIMA ZANZIBAR FEBRUARI 8