SAUDI ARABIA YAJITOSA KUPAMBANA NA UGAIDI

0
232

SAUDI ARABIA, Falme za Kiarabu


SERIKALI ya Saudi Arabia imesema kwamba haitamruhusu mtu yeyote kupata fedha za ugaidi na kueneza chuki na kwamba itashirikiana na Serikali  ya Urusi ili kupambana na vitendo hivyo.

Hayo yalisema juzi na  Waziri wa Mambo ya Nje  wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir, katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati akiwa ziarani nchini Urusi.

“Hatutaruhusu mtu yeyote kueneza  chuki, kutoa fedha za aina ya itikadi hiyo au ugaidi,” alisema waziri huyo.

“Nia yetu ya kukabiliana na vitendo hivyo ni ya dhati, tumewaondoa  maelfu ya maimamu kwenye misikiti kutokana na uharibifu, tunasimamia mfumo wetu wa elimu ili kuondokana na uwezekano wa kutafsiri maandiko vibaya,” aliongeza waziri huyo.

Alisema  ili kutimiza mpango huo, Serikali ya  Riyadh itakuwa ikishirikiana na ya Moscow katika kupigana na ugaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here