26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SARATANI YA TEZI DUME HAITOKANI NA MAGONJWA YA NGONO

NA VERONICA ROMWALD

Ugonjwa wa Saratani ya Tezidume hausababishwi na maambukizi ya magonjwa ya ngono kama wengi wanavyodhani, imeelezwa.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Steven Meena amesema hayo leo alipozungumza na MTANZANIA Digital katika mahojiano maalum yaliyofanyika viwanja vya maonesho ya Sabasaba.

“Katika banda letu jumla ya wanaume 252 wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya tezidume  kati yao 11 walikutwa na dalili za awali za saratani hiyo,” amesema Meena.

Amesema kuwa awali maonesho hayo yalipoanza idadi ya waliojitokeza ilionekana kuwa ndogo lakini iliendelea kuongezeka kadiri siku zilivyosonga mbele.

“Wapo waliotueleza kwamba walihofia kipimo cha kidole lakini baadae idadi iliongezeka nadhani waliokuja mwanzoni walienda kuwaeleza wenzao kwamba tulikuwa tunatumia kipimo cha PSA (cha damu na si kidole,” amesema.

Ameongeza kuwa, ” Mwamko ulikuwa mkubwa na tumebaini bado jamii haina uwelewa wa kutosha kuhusu magonjwa haya ya saratani, kwa mfano walikuwa wanatuuliza iwapo saratani ya tezidume inahusiana na magonjwa ya ngono, yaani mtu anaweza kuipata kwa kushiriki ngono, jambo ambalo si sahihi, tumewaelimisha.

“Pia tulifanya uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake, tumeona jumla ya wanawake 426 kati yao watano tuliwakuta na vivimbe na mmoja tayari alikuwa na dalili za awali za saratani hii,” amesma.

Dk. Meena amesema watu wote waliokutwa na dalili za awali za saratani ya tezidume na matiti wamepewa rufaa kwenda ORCI kwa uchunguzi zaidi na tiba.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles