Samia atoa somo kwa Watanzania waisho Uganda

0
231

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli na wasaidizi wake, imeamua kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wake.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ilisema Samia aliyasema hayo wakati alipokutana na viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Uganda katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort jijini Kampala.

Alisema katika kuleta uchumi wa viwanda, Serikali imedhamiria kuongeza na kuboresha upatikanaji wa umeme, huduma ya maji, kuboresha mitaala ya elimu, kuboresha huduma za afya pamoja na miundombinu.

Aliwaeleza viongozi hao kuwa miradi mingi inayofanyika Tanzania inafanyika kwa kutumia fedha za ndani.

Pamoja na mambo mengine, Samia aliwataka Watanzania waishio nje ya Tanzania kuwekeza nchini kwani kuna maboresho mengi ya kuvutia wawekezaji yamefanyika.

Kuhitimisha mkutano wa Africa Now Summit 2019, Samia alipata nafasi ya kuchangia katika suala zima la mtazamo wa kijinsia.

Alisema bado wanawake hawapewi nafasi ya kutosha kwenye mambo mengi ya msingi kuanzia kwenye elimu, uongozi na masuala mengine ya huduma za kijamii.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, alisema kuna Watanzania zaidi ya milioni 2 wanaishi nchi za nje, hivyo amewaomba kuwa mabalozi wazuri wa kuisemea nchi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here